Saturday 12 October 2013

ZISOME HIZI KUIMARISHA MAHUSIANO YAKO NA MWENZA WAKO


Watu Wengi Ambao Wako Kwenye Uhusiano Wanalalamika Kuwa Wenzi Wao Hawawaoneshi Upendo Kama Ilivyokuwa Siku Za Mwanzo Za Uhusiano Wao. Wanaeleza Kuwa Wanaona Uhusiano Wao Unalegalega Na Mapenzi Yanapungua Taratibu Kama Barafu Iyeyukavyo Juani.

Ili Kuepuka Yote Haya, Hauna Budi Kujifunza Njia Za Kuwasha Upya Moto Wa Upendo Kila Wakati Kwa Kuongeza Ukaribu (Intimacy) Kati Yako Na Mwenzako.

Zifuatazo Ni Mbinu Zitakazokusaidia:

1. Kucheka Pamoja

Kicheko Ni Mlango Wa Ukaribu, Kama Mwaweza Kucheka Pamoja Basi Mwaweza Kulia Pamoja, Na Hapa Mwaweza Kuaminiana Zaidi Katika Kuwasiliana Hisia Zenu, Kama Waweza Kuitofuta Furaha Katika Kila Kitu Basi Unaweza Kupenya Katika Vyote. 

Usiwe Mgumu Na Mwenye Msimamo Mkali Katika Kila Kitu. 

 Jifunze Kujizuia Pale Unapoanza Kuelekea Kwenye Kukasirika Na Badala Yake Tumia Kucheka Kama Mlango Wa Kutokea. Kama Utaanza Kujizoeza Hivi Ukiwa Nyumbani, Taratibu Utaweza Ukiwa Ofisini Na Hata Kwingine Kokote.





2. Jifunzeni Kutiana Moyo

Kila Mmoja Awe Msaada Na Tegemeo Kwa Mwenzake. Jifunze Kumtia Moyo Na Kumwezesha Mwenzako. Sikiliza Na Kufuatilia Vile Mwenzako Afanyavyo Au Apendavyo.

Onyesha Heshima Katika Vitu Hivyo Pia. Kila Upatapo Nafasi Mpongeze Mbele Za Watu Au Hata Unapokua Nae Peke Yenu. Mjenge Mwenzako Mbele Ya  wengine Na Kubali Pongezi Zote Za Mafanikio Yenu Zimwendee Yeye. Mruhusu Mpenzi Wako Ajue Kuwa Una Mkubali Katika Kila Afanyalo. Zaidi Tunavyo Wainua Wapenzi Wetu Ndivyo Wanavyotuthamini Na Kutunyanyua Na Sisi Pia.

3. Jifunzeni Kupenda Kugusana

Nguvu Ya Mguso Wa Ukaribu Kamwe Haiwezi Kulinganishwa Na Chochote. Lazima Mjifunze Kujenga Tabia Ya Kugusana Mara Mpatapo Nafasi Sio Tu Mnapokuwa Mmelala. Kugusana Huku Ni Pamoja Na Kushikana Mkono Mkiongea Au Mkitembea, Kukumbatia Bega, Kugusa Au Kuchezea Nyewele Za Mwenzako Na Njia Nyingine Zozote Za Kuonyesha Ukaribu Kimwili. Wengi Wetu Huweza Kufanya Haya Kidogo Tunapokuwa Peke Yetu Na Kamwe Sio Mbele Ya Watu, Je, Ni Aibu, Nidhamu Mbaya? Dhambi?
Kugusana Ndiyo Mwanzo Wa Kuamsha Hisia Za Kuhitajiana, (Hebu Jiulize Kisirisiri, Lini Uligusana Na Mwenzako Nje Ya Chumba?). Kumgusa Umpendaye Hukuzuia Kutowaza Kumgusa Yeyote Katika Ulimwengu Uliojaa Wengi Walio Wapweke.

Mguso Huu Wa Upendo Haumaanishi Mguso Wa Tendo La Ndoa, Ingawa Pia Ni Vyema Kujifunza Kuijenga Lugha Ya Mguso Wa Tendo La Ndoa Katika Uhusiano Wenu.



 4. Zungumzeni Hisia Zenu

Kati Ya Vikwazo Vikubwa Katika Ustawi Wa Uhusiano Mengi Hususan Ya Wanandoa Ni Kutokuwepo Kwa Majadiliano. Lazima Wapenzi Wajifunze Kuzungumza Kuhusu Hisia Zao. Kama Vile Maisha Yasivyo Na Ukamilifu, Uhusiano Na Hata Ndoa Pia Hazina Ukamilifu. Mpenzi Wako Hayuko Kamili Na Wala Wewe Pia Siyo Mkamilifu. Jifunze Kuzungumza Na Umpendaye Jinsi Unavyojisikia Na Nini Kinachokusumbua. Kuendelea Na Migogoro Isiyosuluhishwa Husababisha Moyo Kuwa Baridi Juu Ya Mwenzako. Jiwekeeni Muda Kila Wiki Wa Kutoka Ili Kuzungumza Mambo Yenu. Mwambie Umpendaye Yapi Yanayojiri Kila Siku Na Zipi Ni Changamoto Zako Mkiweza Kujifunza Kuwekeza Katika Muda Wa Kuwa Pamoja Taratibu Hata Muda Wenu Wa Maongezi Ya Simu Utaongezeka.

5. Samehe Na Kubali Kusamehewa

Kamwe Tusiache Maumivu Na Machungu Yatawale Uhusiano Wetu. Lazima Tujifunze Kuwasamehe Tuwapendao Na Kujisamehe Sisi Pia. Kutofautiana Katika Uhusiano Kupo Sana, Na Lazima Tuwape Tuwapendao Nafasi Ya Kuelezea Vile Vinavyowaudhi Dhidi Yetu. Kila Hisia Za Mmoja Wetu Zina Umuhimu. Huwezi Kujiona Vile Ulivyo, Mruhusu Mwenzako Akwambie Yanayomuumiza Na Msameheane.

6. Linda Mwonekano Wa Mpenzi Wako

Mara Nyingi Hatari Hii Hutokea Tunapokuwa Katika Mizunguko Ya Huku Na Huko. Ukaribu Na Mpenzi Wako Hauendelezwi Tu Bali Unalindwa. Mwonekano Wetu Lazima Uwe Halisi Na Siyo Bandia . Vile Tunavyoviona Katika Tamthiliya Na Filamu Siyo Ukaribu Ulio Halisi. Kama Tunataka Tuonekane Sawa Na Vile Tunavyowaona Wengine Wanavyopendana Basi Tunakosea Na Kujizuia Kuwa Na Mtazamo Bora Katika Uhusiano Wetu. Ukianza Kupata Ukaribu Wa Kweli Baina Yako Na Mwenzako, Utapoteza Hisia Ya Kuhitaji Ukaribu Huo Na Mwingine Yeyote, Na Badala Yake Utaanza Kuulinda Ukaribu Mlionao.

Lengo Liwe Kuvitafuta Vile Vyote Mpenzi Wako Alivyonavyo Ambavyo Ni Kukuza Ukaribu Wenu. Mwenzako Awe Ndiyo Mtu Wa Muhimu Kuliko Wote Katika Maisha Yako.


MWANAMKE ANAHITAJI NINI........



Mwanamke Ana Upendo 98.8999% Kwa Mwanaume…Mwanamke Mpaka Kufikia Hali Ya Kukubaliana Na Wewe Na Akakuheshimu Kwa Kukuvulia Kilakitu Alichonacho Yeye Kwa Kukupa Kile Wewe Unachohitaji Kutoka Kwake Na Amekupa Heshima Wewe Kama Mpenzi Wake Umtumie Unavyokata Na Kutokana Na Mapenzi Anayokupa Anaamua Kukuamini Na Kukupa Siri Zake Zote Wewe Kama Wake Mpenzi Na Mpaka Anawatambulisha Rafiki Zake Kuwa Wewe Ni Shemeji Yao Na Hawezi Ambiwa Chochote Juu Yako Kibaya Akaacha Kukwambia, Then Leo Hii Unamdharau “Aahgghr! Hana Lolote Huyo Kwanza Malaya Tu” …(Mbaya Sana Hii, Jifunze Kuishi Kiutu Uzima Hata Kama Ana tofauti Usiwe Na Hofu Kumweleza Na Ninaimani Atakuelewa)

Usimtese Kijinsia , Usije Thubutu Kumuacha Na Kasoro Zake , Ninamaanisha Kwamba Kama Anatatizo Au Wakati Wa Mambo Yetu Yale Kuna Kitu Unataka Ufanyiwe Na Yeye, Labda Yawezekana Hajui Au Anajua Lakini Ana Walakini Kukifanya, Basi Ni Lazima Umweleze, Muweke Wazi Kumbuka Huyo Ni Mpenzi Wako Ukiwa Kimya Ukasubiri Raha Ukapewe Na Kimada Wa Nje Basi Utajikuta Siku Ya Mwisho Unaleta Ugonjwa Ndani Au Wewe Kukusababishia Kukosa Nguvu Za Kiume Unapokutana Naye Mara Nyingi Kwa Sababu Ni Chanzo Kingine Cha Kusababisha Kukosa Nguvu Unapotembea Na Wanawake Wasiohesabika, Ukikutana Naye Mara Inalala Hii Ni Kutokana Na Uchapaji Wa Too Much Nje, Kwa Sababu Unapokuwa Naye Huwezi Ku Feel Kuwa Naye. Na Badala Yake Utaanza Kuwawaza Wengine Wa Nje Ambao Hawatakusaidia Katika Kujenga Uhusiano Mwema Na Mpenzi Wako. (Kumbuka: Hata Ukibadilisha Kuni, Moto Ni Ule Ule)
Mwanamke Akikupenda Usimdharau Kama Yeye Ni Malaya… Na Mwanamke Mpaka Ukiona Hajatulia Basi Jua Tatizo Lako Wewe, Fanya Juu Chini Ili Kuweza Kumbadilisha Kwa Sababu Kumbadilisha Mwanamke Ni Kitu Kidogo Sana Kwa Sababu Umekaa Naye Muda Mrefu Na Ni Lazima Utajua Tu Umguse Wapi Aweze Kuwa Kama Mwanzo, Kama Umeshanifuatilia Kwa Mada Zangu Ninazokupa Kupitia Hapa . Na Usijeomba Mwanamke Akulilie Machozi Mbele Zako, Ameshindwa Kumlilia Baba/Mama Yake Aliyemzaa Na Amekuja Kukulia Wewe… Wewe Una Nini? Epukana Na Hili Na Utunze Heshima Yake Na Umpe Penzi Lako, Hakuna Mwanamke Mbaya/Malaya/Kicheche Ila Wewe Ndio Utafanya Awe Hivyo… Wengi Wao Wameshawahi Kufanya Haya Na Sasa Wanalia Na Kusaga Meno Kwa Sababu Walijisahau Na Mwishowe Sasa Hawajielewi Kutokana Na Maisha Wayoishi Ya Kutokua Na Chaguzi Zilizo Za Halali…

Mwanamke Anapenda Kupendwa! Mara Nyingi Wanawake Ndiyo Hasa Huwa Na Mapenzi Ya Dhati Zaidi Kuliko Wanaume. Mwanamke Anapoamua Kuwa Na Mpenzi Wake, Humpenda Kwa Moyo Wake Wote, Hivyo Hupenda Kuwa Salama Katika Penzi La Dhati Kwako.

Anapenda Uhuru, Anapenda Kujisikia Wazi Kwako Mahali Popote. Mwanamke Anajisikia Vibaya Sana Anapokuwa Hana Uhuru Hata Wa Kukushika Mkono Mnakuwa Barabarani Pamoja. Anapenda Penzi La Uwazi!

Maana Mwingine Utakuta Akikutana Na Rafiki Yake, Badala Ya Kumtambulisha Vizuri Kama Mpenzi Wake, Anaanza Kupatwa Na Kigugumizi. Utamsikia Akisema: “Ah! Huyu Ni Rafiki Yangu Bwana, Anaitwa Latipha....”Hili Ni Kosa Kubwa Linalofanywa Na Wanaume Wengi Bila Kujua Ni Kosa.

Mwanamke Anakosa Amani Ya Moyo Kutokana Na Unavyomtafsirisha Mbele Ya Rafiki Zako. Anahisi Hayupo Salama. Lazima Atajiuliza Maswali, Kwanini Hataki Kunitambulisha? Kwanini Anashindwa Kusema Mimi Ni Mpenzi Wake? Sifananii? Sina Mvuto Au Nina Tatizo Gani?

Hayo Yanaweza Kuwa Maswali Yatakayomuumiza Sana Kichwa Mpenzi Wako, Ambaye Si Ajabu Akafanya Maamuzi Ambayo Hutayapenda. Kidonda Hiki Hubaki Moyoni Mwa Mwanamke, Huwa Vigumu Sana Kuonyesha Wazi Kwamba Amechukia Kutokana Na Uliyomfanyia, Lakini Atabaki Akiugulia Moyoni Mwake Kwa Uchungu.
Hata Hivyo, Kinachokuja Akilini Mwake Ni Kutafuta Mwanaume Mwingine Ambaye Atakuwa Wazi Kwake Ili Aweze Kufurahia Mapenzi Badala Ya Kuendelea Kuumia Moyoni Mwake. Ni Dhahiri Kwamba Uamuzi Huu Hautaufurahia Hakika.
1. UNAVYOJALI...
Mwanamke Anapenda Awe Wa Pekee Kwako, Umsikilize, Umjali Na Umpe Kipaumbele Katika Kila Unachokifanya . Wanawake Wengi Wanapenda Kudekezwa, Lakini Hawapendi Kuweka Hilo Wazi Kwa Mwanaume Wake. Kwa Kumtazama Tu Utagundua Mpenzi Wako Anahitaji Nini Zaidi Kwako!

Wakati Mwingine Anaweza Kukupa Mitihani Ili Kupima Kiwango Cha Penzi Lako. Anaweza Kukuambia Anaumwa Au Anauguliwa Na Mtu Wake Wa Karibu, Lengo Ni Kuangalia Ni Jinsi Gani Unakuwa Makini Anapokuwa Na Matatizo.

Vile Utakavyochukulia Tatizo Lake Kwa Ukaribu, Uchungu Na Kuona Kama Lako, Ndivyo Utakavyomfanya Aone Thamani La Penzi Lako Kwake, Ikiwa Vinginevyo Basi Humuacha Na Machungu Moyoni, Huku Akijutia Kuwa Na Mpenzi Wa Aina Yako.

Hii Ni Siri Ambayo Si Rahisi Mwanamke Wako Akueleze Moja Kwa Moja. Atatumia Lugha Ya Ishara Kuonesha Jinsi Ambavyo Anahitaji Kuwa Wa Pekee Kwako.

2. JIFUNZE SIRI HIZO.....

Hapa Ndipo Mwanaume Mwerevu Anatakiwa Kuwa Makini, Ni Lazima Ufahamu Siri Zilizopo Moyoni Mwa Mpenzi Wako. Jifunze Kusoma Hisia Za Mpenzi Wako Kwa Nje, Kabla Ya Kufanya Kitu, Fikiria Mara Mbili, Lakini Baada Ya Kufanya, Msome Kupitia Uso Wake.

Analifurahia Au Umemchukiza? Ni Vizuri Kugundua Hilo Ili Uweze Kufunga Hisia Za Kumfanya Aanze Kufikiria Kukusaliti. Hata Mnapokuwa Faragha Ni Vizuri Kuwa Makini Na Kila Unachokifanya! Chunguza Kama Anafurahia Penzi Lako Na Manjonjo Yote Unayomfanyia.

Kumbuka Kwamba Ni Vigumu Sana Mwanamke Kukueleza Moja Kwa Moja Kwamba Hujamfurahisha Au Kuna Kitu Umekikosea, Hii Husababishwa Na Hofu Ya Kuogopa Kukufanya Ujisikie Vibaya.

Kwa Maneno Mengi WEWE Mwanaume Ndiye Mwenye Kazi Ya Kuangalia Mwanamke Wako Anapenda Nini Na Nini Hapendi Ili Uweze Kuwa MWANAUME Wake Bora, Maana Hata Hisia Zake Za Ndani Utakuwa Unazifahamu. Ni Rahisi Sana, Soma Kupitia Macho Yake Kila Unachomfanyia, Utaujua Ukweli. Unajua Hata Ukimwita Kwa Jina Ambalo Hana Msisimko Nalo Lakini Ukiwa Unamtazama Usoni Ni Rahisi Sana Kugundua Kitu Fulani, Kama Hajakipenda Utaona Kwenye Macho Na Akikipenda Pia Utaona.

Unapokuwa Naye Faragha, Tumia Uwezo Wako Wote, Lakini Kumbuka Kwamba Si Kila Utakachokifanya Utamfurahisha. Hii Inamaanisha Kwamba, Baada Ya Kumchunguza Jinsi Anavyosisimka, Utaweza Kugundua Wapi Kuna Msisimko Zaidi Kuliko Sehemu Nyingine.

Hapo Sasa Unaweza Kuibuka MSHINDI Maana Utakuwa Umeziweka Siri Zake Hadharani, Kwa Maneno Mengine Kama Yeye Aliona Siri, Basi Umeweza Kuzigundua Na Angalau Umeanza Kuzifanyia Kazi. Nawapenda Sana Rafiki Zangu, Ndio Maana Nawapeni Mambo Mazuri Na Yenye Sifa Ili Msiweze Kusababisha Kitu Kinaitwa..."UMENITENDA/AMENITENDA" (KUTENDANA NI DHAMBI KUBWA SANA) NIWATAKIE SIKU NJEMA..

WAZO LA LANGU LEO:

WANAWAKE: Napenda Kuwashauri Wanawake Wote Ambao Wapo Katika Mahusiano Ya Kimapenzi Wajaribu Kuwa Wabunifu Katika Mapenzi, Mpe Mpenzi Wako Mapenzi Yote Toka Moyoni Mwako. Usidanganywe Kuwa Mapenzi Ni Mitishamba Hakuna Dawa Ya Mapenzi Kwa Mganga Ila Dawa Unayo Wewe Mwenyewe Mridhishe Mpenzi Wako Kwa Kumpa Vitu Vipya Katika Mapenzi Halafu Uone Je, Penzi Lako Kwa Mwenza Wako Utachangia Na Wenzako?!

WANAUME: Siku Zote Uwapo Katika Mapenzi Fahamu Kuwa Unapaswa Kumridhisha Mpenzi Wako Katika Tendo Mfanye Ajisikie Raha Pindi Muwapo Chumbani Inakubidi Uwe Mwanamke Wa Kileo Ujitahidi Kuwa Mbunifu Katika Mapenzi Kwa Kujituma Pindi Mnapokuwa Chumbani Na Mpenzi Wako, Jaribu Kushughulika Tumia Viungo Vyako Vya Mwili Katika Kuamsha Hisia Za Mwandani Wako Kabla Ya Kuanza Nae Kufanya Mapenzi Ili Kuhakikisha Mpenzi Wako Anapata Raha Na Inakuwa Ni Njia Nzuri Ya Wewe Kumfanya Mpenzi Wako Ahisi Kuwa Wewe Ni Muhimu Kwake.

No comments:

Post a Comment