Tuesday 29 April 2014

soda inayowezakumfanya mwanaume kuwa tasa

Kinywaji cha coca cola kimeendelea kuwa maarufu duniani lakini utafiti mpya umeonyesha kuwepo uhusiano wa kunywa sana kinywaji hicho na matatizo ya uzazi kwa wanaume.
 
Kwa mjimu wa utafiti huo uliochapichwa kwenye Jarida la Epidemiology la Marekani, wanaume wanaokunywa zaidi ya lita moja ya coca cola kwa siku wanakabiliwa na hatari ya kuwa tasa. Wanaume waliotumia kinywaji hicho walikuwa na upungufu wa aslimia 30 ya mbegu za uzazi zilizohesabiwa, ikilinganishwa na wale ambao hawakutumia. 
 
Wanaume hao walionekana kuwa na matatizo ya uzazi zaidi kuliko wasiokunywa coca cola.

SIRI YA TATOO KWA WANAWAKE....



                                     tattto mapajani na mgongonii
Tattoo ni michoro mbali mbali inayo chorwa kwenye mwili wa myamaa hasa mwanadamu,wengi ujiuliza kwa nini watu wana wake kwa waume huchora tatu ? Jibu kubwa kulingana na utafiti ni tattoo huwa moja ya
urembo kwenye miili yao.
Wanawake wao wameonekana kuchora tattoo hizo kwenye sehemu zaonza siri zaidi kuliko sehemu za kawaida za mwili wao na watu hujiuliza nini sababu kubwa?? JIbu ni urembo unaopendezesha na kuvutia zaidi wanaume{kimapenzi} pale endapo wakiona sehemu hizo za siri zikiwa zimepambwa na tattoo.

DENTI MWINGINE AACHIA PICHA ZAIDI YA 10 MTANDAONI HUYU NDIO KAFUNIKA WOTE HUWA WANATANIA TU ANGALIA HAPA LEO

 LIKE PAGE YETU KWANZA KISHA CLIK HAYO MANENO CHINI HAPO

Saturday 29 March 2014

SIKIO HALISI;

Mambo muhimu ambayo unatakiwa uyafanye kabla ya kuoa au kuolewa.
 

Pastor, Gordon Kalulunga.


MOJA ya mambo ambayo yanakosekana katika nyumba za ibada ni mafundisho ya mahusiano.

Watu wengi hawajui kuwa mtu aliyeolewa na hajaolewa au kuoa, ana haki ya kupata elimu ya ndoa.

Unaweza kujiuliza kuwa kwanini ndoa nyingi zina shida? Jawabu ni kwamba wengi wanajua ndoa baada ya kuingia kwenye ndoa, hawajawahi kupata elimu ya mahusiano.

Ni sawa na kumfundisha dereva kuendesha gari.

Wengi wamekosa elimu ya mahusiano au kuoa au kuolewa, vijana na mahusiano, bali wengi wana elimu za upako wa mafanikio na toa ndugu toa ndugu ndiyo masomo tuliyoyazoea.

Mfumo wa elimu tuliyonayo nao ni tatizo. Kwa mfano kwenye Biblia hakuna neno linalosema rafiki au mchumba.

Huwezi kukuta kitu kinachoitwa, urafiki, uchumba baadaye ndoa.

Ngoja nikuambie, Mathayo Mtakatifu sura ya 1;1-23. Mariamu alipoposwa….. haisemi alichumbiwa! Lakini katika utamaduni wa kimagharibi leo hii watu wanasema kuwa mchumba wa Yusufu.

Mchumba huwa anapimwa, ndiyo maana watu wanakuwa na wachumba wengi kweli na hatimaye uchumba unavunjika kwasababu hakuna mtu anayeenea kwenye utimilifu.

Kuna fix za kifikra ambazo zina ugonjwa wa kufisha, kesho unaweza kulia ukiendekeza kumtafuta mchumba badala ya kumtafuta mume au mke.

Akina dada wengi wanaomba na kusugua magoti wakiomba wapate wachumba.

Maandiko yanasema kuwa, ‘’Mjibu mpumbavu kutokana na upumbavu wake’’
Mtu ana wachumba kadhaa, kisha anaanza kumuomba Mungu ampe mume au mke huku akiwa na vinyago vyake. Majibu yatakuja kama anavyowaza. 

Yaani tayari wana fikra, vinyago na maamuzi yao kati ya wale wachumba waliopo moyoni na kichwani.

Mungu atamjibu mtu kutokana na elimu aliyonayo ya urafiki, uchumba kisha ndoa.

 Walio kwenye ndoa wengi wanajuta kwasababu wameoa au kuolewa na rafiki….

Ukikaa na mtu utasikia anakuambia, mtumishi nimeumia, tunakuabudu Bwana, utafikiri upako umetembea, kumbe watu wana kesi zao na nafsi zao zimepigwa.

Mimi kama mwalimu ambaye sawa na Daktari, nikianza kufuatilia ninajua.
Ukimuuliza vipi ina maana una chimichimi ya roho mtakatifu ndiyo maana kila tunapoanza kuabudu analia?

Ukidadisi mtu anakumbia kuwa, nilikuwa na mchumba akaniambia utanioa, akamwambia na rafiki yangu na mwingine…..

Nafsi za watu wa Mungu nyingi zimeumizwa na kuna kesi nyingi za kuachwa kuliko kesi za uhalifu mwingine.

Ukiomba mchumba, wanaweza kuja wengi kisha unapoanza kuburuzana nao unachoka kisha unatumbukia popote…..

Jambo hili la ndoa na uchumba ni gumu kwasababu vijana wengi ni wavivu kujifunza maandiko ya Mungu bali wanataka watafuniwe kila kitu na kulishwa.

Mungu ni roho, alimuumba mtu kwa mfano wake, akasema nendeni duniani mkazae na kuongezeka. Maandiko yanaposema Mtu, ina maanisha mfano wa roho.

Kwenye ulimwengu wa roho, Mungu aliumba mtu mke na mtu mume na ndiyo maana amekataza kuzini.

Maana yake ni kwamba kila mmoja ana mke wake na ana mume wake kwasababu kila mmoja aliumbwa na wake.

Ukiishika elimu hiyo, hautalia kwasababu eti hujapata mume au mke. Mbinguni kuna roho nyingi zinazataka kuja duniani, hivyo tuliopo tumepata neema ya kutangulia kuzaliwa.

Unapomuona mwanaume anapita, ujue kuwa huyo ni mume wa mtu na mwanake anayepita ni mke wa mtu.

Tatizo watu wanaomba kwa Mungu wapate mke au mume huku wakilia! Inashangaza mtu unaenda kudai deni lako huku akilia. Maana yake hajui haki yake, yaani imani zetu hazijawa sawa.

Kama ndani yako una usongo wa kuoa au kuolewa, fanya hivi. Kwa imani nenda kamnunulie na suti iweke ndani maana kwa imani yupo. Acha kushika yeyote mwisho utashika hata majoka.

Mungu hupendezwa na mtu mwenye imani na anamletea. Acha kulia.

Wanaume ngoja niwaambie. Mungu alipokuwa akiumba, alimtanguliza Brother men, kisha akamlaza usingizi na kuchomoa ubavu akamtengeneza mwanamke. Maana yake ni kwamba mwanamke wa kwako yupo, labda uwe towashi.

Wanawake hampaswi kufifia ngozi kwamba hamtaolewa, maana usigeweza kuumbwa bila wa kwako kuwepo na wala hajafa bali yupo, cha kufanya amini. Kanunue na suti kaweke ndani, anza kufanya maandalizi…

Kuweni na imani inayowekwa kwenye matendo, msiamni kuwa mtakosea.

Sehemu nyingine huwa nawafundisha kuwa, ukishatambua kuwa wa kwako yupo, tulia au subiri.

Kwa kuwa hatuamini kuwa wa kwako yupo, hatutulii, na kwa kuwa tunaanza kaba ya majira na wakati ndipo tunapoeekea kwenye kuumia na majuto ya uchumba na ndoa.

Wimbo uiobora 3;5 ….msiyachochee mapenzi wala kuyaamsha……Mungu anasema hayo kwasababu kabla ya Mungu kuyaamsha, wewe unawahi.

Mfano; Sekondari mtu hasa wanawake, anapokuwa kidato cha pili tu au kabla ya hapo, anaanza kuomba, Mungu nipe Mume….. hebu jiulize wewe ulianza lini kuzitikisa mbingu za mapenzi…… jibu unalo.

Wanyakyusa wanao usemi kwa mtu mzima anayefanya mambo ya hovyo, unasema…..amakambo, akwesile ndili… yaani mtu huyo anasumbuliwa na bangi….alivuta lini?

Hapa namaanisha kuwa unaweza kukimbilia na ukapata mume maana hakuna mtu anayekuwa anazijua tabia za wenzake, kisha utaanza kusema kuwa aaaaa…kumbe hakuwa mwenyewe..

Ibrahimu haraka zake zinasumbua kule Israel mpaka leo. 

Niwaambie ukweli kuwa haraka zina hasara zake sawa na utunzaji wa mtoto njiti ni kazi kubwa. Hivyo ukiharakisha unaweza kupata mume au mke njiti…

Sijui kama ninaeleweka katika somo hili. Haraka zinaendana na akina dada kuongea harakaharaka, wanaume wengi hawapendi mwanamke wa namna hiyo.

Yesu aliwahi kujaribiwa na kahaba, mafarisayo miili yao ikawa nyang’anyang’a huku yule kahaba akitoa machozi na kufuta miguu ya Yesu kwa nywele zake, hivi ungekuwa wewe Brother men ungefanyaje hapo?

Usiwe na haraka. Watoto wa kike ndo wana speed kuliko hata dunia inavyozunguka jua.

Hamnoni alimpenda Tamali mpaka akaumwa…. Lakini baada ya kulala naye akamchukia na kumwambia Tamali aondoke na akamchukia kwelikweli…..tafakari.

Hapa kinachotendeka katika ulimwengu wa roho ni kependa umbo lakini my akionja hakuti kile ambacho alikuwa anakifikiri.

Mfano mzuri ni kwamba wanaume na wanawake wengi ambao wamedumu katika mapenzi hawaoani.

Mwanaume akitembea na mwanamke na kutokukuta alichokitarajia, anasema hata kwa wenzake kuwa ‘’demu mwenyewe mshamba na hana lolote’’ yote hiyo ni kuyachochea mapema na kuvua. 

Nitajuaje kama ndiye?

Kimaandiko unapomuomba Mungu, utawekewa rohoni kitu kinachoitwa mwongozo.

Utaona unasukumwa na jambo la kuolewa kama kuku navyosumbuka kutafuta eneo la kutagia, sawa na mtumishi wa Mungu anapotaka kufanya jambo la kiroho.

Jifunze kumsikiliza Mungu, ondoa moyoni kufikiri kuwa huyo unayefikiri na kumweka moyoni kama ni mwenyewe, huyo siyo. Achana naye maana roho ya mauti ipo juu yako. Tubu.  

MSIKILIZE MUNGU ILI ASIKUJIBU SAWA SAWA NA VINYAGO ULIVYOWEKA MOYONI MWAKO NA KUJIINGIZA POPOTE. 

HEBU JIULIZE, MPAKA SASA UNA VINYAGO VINGAPI?
Hili ni somo la sikio halisi, siku nyingine nitatoa mifano yangu halisi…..
Mungu awabariki na awasamehe wote wenye toba.


Gordon Kalulunga
Information and Media Consultant
P.O. Box 705, Mbeya-Tanzania
Tel: 255 (0)754 440749
WEB; www.kalulunga.blogspot.com

Saturday 22 February 2014

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2013 HAYA HAPA

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani  la Tanzania,  Dk. Charles Msonde, akitangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT), Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Naibu Katibu Mtendaji wa  baraza hilo, Edward Haule. (PICHA NA KHAMIS MUSSA)

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2013 KWA MKOA WA MBEYA BOFYA HAPA CHINI KUTAZAMA MATOKEO YA SHULE

ST. FRANCIS GIRLS SECONDARY SCHOOL

















































Kupata matokeo ingia kwenye tovuti ya NECTA ya: 

http://www.necta.go.tz/index.php 

Kisha bofya sehemu ilioandikwa MATOKEO YA CSEE 2013 & MATOKEO YA QT 2013 Upande wa juu  kulia pembeni mwa tovuti

Thursday 20 February 2014

WABUNGE WA KATIBA MPYA KUTAKA NYONGEZA ZA POSHO, SIRI NZITO YAFICHUKA


*Wabunge wa Jamhuri wadaiwa kuwa kichocheo
Kalulunga blog team, Dodoma.

SIKU moja baada ya wabunge maalum wa bunge la katiba kulalama na kutaka kuongezewa posho, uchunguzi umebaini kuwa shinikizo hilo linatokana na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



Baadhi ya Wabunge hao wa Jamhuri, wanadaiwa kusukuma jambo hilo kwa maslahi yao binafsi na kwa malengo yao ambayo tayari yamebainika.



Malengo yaliyotajwa na vyazo vyetu vya habari, vimesema kuwa wabunge hao wanashinikiza wabunge wa bunge maalum waongezewe posho kutoka kiwango cha sasa cha Tsh. 300,000 mpaka kufikia kiasi cha Tsh. 540,000 kwa siku.



Vyanzo hivyo vinahoji iweje wabunge hao walioomba kufanya kazi hiyo kwa maslahi ya taifa wadai kiasi hicho kikukwa cha fedha!



‘’Hawa wamekuja hapa kwa maslahi yao na hata katiba itakayopitishwa hapa itakuwa kwa maslahi yao na wala si wananchi’’ kilihoji moja ya chanzo chetu kutoka miongoni mwa walengwa wanaopinga ongezeko la posho hizo.



Aidha uchunguzi umebaini kuwa, nia kuu ya wabunge wa Jamhuri wanaoshinikiza ongezeko la posho hiyo, wanalenga kupata mkupuo wa fedha ambazo zitawawezesha kulipa ama kupunguza madeni ya magari yao ya kifahari waliyoyakopa.



Wakati hali hiyo ipo hivyo, taarifa kutoka serikalini, zimeeleza kuwa mpaka kufikia leo, Halmashauri kote nchini, bado hazijafikishiwa fedha za maendeleo ya wananchi.



''Wanatumia mwanya wa bunge la katiba kutaka nyongeza ya posho ili kulipa madeni ya magari yao''.