Friday 11 October 2013

WANAWAKE WALIOOLEWA AU WANAOISHI NA WANAUME WANASTAHILI KUPEWA SIFA, SOMA HAPA

Hebu fikiria:

ANAKUFUMANIA:
Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza, anakuelewa,anakusamehe - halafu anasahau.
UNAZAA NJE YA NDOA: 
Anasononeka na kulia sana. Anachukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo.
 
UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI:
Anakukaribisha, anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.
 
UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER:
Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake) Unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!
 
CHAKULA CHA USIKU: 
Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho
yake tena inaweza kutokea. Hana kinyongo!
 
UNAJIANDAAA KWENDA KIBARUANI: 
Unakuta kashakuandalia viwalo, suruali imenyooshwa kama
ya askari trafik, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana kashasahau na kukusamehe!
 
UNAMPA UJAUZITO: 
Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuachia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena! Na mengine meeeenggggiiiiii sana wanafanyiwa hawa watu lakini
 
WANASAMEHE, WANAVUMILIA! 
Ni watu muhimu sana hawa....!
HIVI INGEKUWA WANAUME WANAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?

No comments:

Post a Comment