Thursday 26 December 2013

MACHO HUONYESHA HISIA KATIKA MAPENZI

unaweza kuwa na hasira,,mawazo,,ama furaha na macho yako yakaonyesha ishara bila kificho lakini pia katika suala zima la mapenzi hisia huonekana machoni





yapende macho yako wakati wote na pia tumia macho yako kufahamu hisia za mapenzi ya mwenza wako

Monday 2 December 2013

PICHA YA LEO

MDAU ANATAFUTA RAFIKI WA KIKE

BAADA ya kusoma blog yako usiku huu, naomba nitafute rafiki wa kike (miaka 30-35). Unene, urefu wa wastani, rangi yeyote, kupitia blog yako brother kalu.

Age yangu ni miaka 40. Akipatikana naomba atume sms kwenye namba hii 0789 431774

SALAAM KUTOKA KWA MDAU

Niaje Brother Kalu? 0714637957.

JIBU; poaaaaaa...

SWALI KUTOKA KWA MDAU DANDA WA MASWA

JE nikiwa mbali na mpenzi wangu kwa muda mrefu tunaweza kupoteza mahusiano yetu? Naomba ushauri wako.

JIBU NI KWAMBA KAMA ILIVYO KAWAIDA KWA ANAYEHITAJI USHAURI TULIWEKA UTARATIBU WA KUTUMA 10,000/= ILI UWEZE KUPATA SHAURI WA MAHUSIANO. 

LAKINI WEWE HAUJAFANYA HIVYO WALA HUJAWEZA KUAPATA MAELEKEZO YEYOTE.

MDAU ANATAFUTA MCHUMBA

Natafuta mchumba mwenye umri wa kati ya miaka 18, awe mnene kwa chini juu awe wa kawaida asiwe mweupe sana. 

Namba yangu ni 0788 446374

Saturday 26 October 2013

KANUNI ZA KUEPUKA KUZINI NJE YA NDOA AU MPENZI WAKO

Hakunaga na Brother Kalu
Kanuni za kuepuka kuzini nje ya Ndoa au mpenzi wako
Leo tuende moja kwa moja kuangalia baadhi ya mambo ambayo yaweza kukusaidia kuepuka kuzini nje ya ndoa yako au kutoweza kumsaliti mpenzi wako.
1.      Kujiepusha kuwa karibu na jinsi zingine ukiwa umelewa
Hapa nitoe ufafanuzi wa jambo moja la jinsi ambapo nazungumzia masuala ya maumbile ambapo wengi wetu tunachanganya neno jinsi na Jinsia.
Kuepuka kuwa karibu na jinsi tofauti nawe ni suala gumu sana lakini ni vema unapokuwa unakula maji(kilevi) ni vema ukawa makini kuwa mbali na mtu wa jinsi nyingine ili kuepukam kupata vishawishi na kumsaliti mwenzi wako.
2.     Epuka mazungumzo ya kimahaba
Ni njia rahisi sana inayoshawishi watu wengi kujiingiza kwenye usaliti ama mapenzi mapya ambapo endapo hautakuwa makini na kujiingiza katika mazungumzo ya kimahaba na mtu wa jinsi nyingine unaweza kujikuta unajiingiza katika usaliti wa kimapenzi lakini nji hii licha ya kuwa ni njia moja wapo ya kuepuka usaliti ni njia nzuri ya kuanzisha mapenzi mahusiano mapya ambapo wengi hushawishika na kujikuta kutamani kupata vitu vipya katika mahaba ambavyo mtu aliyenaye kwa muda huo amevigusa katika mazungumzo yao.
3.Kuwa mkweli
Ukweli ni jambo muhimu katika kudumisha mahusiano na kuepuka usaliti kwasababu mwenzi wako anaweza kuhisi kitu kuwa umeanzisha mahusiano na mtu mwingine ambaye mara kadhaa mnafanya nae utani, hivyo ni vema ukawa mkweli kwa mwenzi wako kumweleza kuwa mtu huyo mnafanya masihara nae na wala hakuna jambo lolote linaloendelea kimahusiano tofauti na kutumia lugha kama ‘’Kwani unafikiri mimi nafanya nini nae’’ hilo jibu sahihi katika kuboresha mahusiano yenu.
4.Epuka kupigana busu na jinsi nyingine
Kumpiga busu mtu ambaye si jinsi moja nawe ni kichocheo cha usaliti katika ndoa na hata mapenzi ya kawaida kwasababu Mungu aliumba miili yetu katika misisimuko ya aina mbalimbali ambapo mtu mwingine ukimpiga busu bila kujalisha kuwa ni mwanaume au mwanamke hujikuta anasisimuka vibaya sana na kuhisi kuwa angekuwa sitakwa sita nawe kwa muda huo angesisimuka hivyo si vema kufanya hicyo.
5. Usimweleze mtu hisia zako
Epuka kueleza hisia zako za kimahaba kwa mtu asiye wa jinsi yako kwa mfano mtu kagombana na mpenzi wake ama mke/mume wake si vema ukamwambia hisia zako kwake za kutomtenda bali ni vema kumwambia kuwa siyo vizuri kugombana na mwenzi wake na jaribu kutoa ushauri ambao hauna ushawishi wa kumwondoa kwa mwenzi wake.
Hapa sielezi kuwa haupaswi kuwa mkarimu kwa watu la hasha bali nazungumzia kuwa makini na kuepuka kuwa mmoja wa watu wenye historia za kuvunja mahusiano ya watu bali ukiwa mshauri mwema utaheshimika zaidi.
6. Onyesha wajibu wako
Ni vema katika mahusiano kila upande ukaonesha wajibu wake kwa mwenza wake ambapo waweza kumtia moyo mwenzi wako kuwa yeye amekuwa sumaku kwako kwa kukupa faraja na hasa ni mwanamke/Mwanaume  ambaye ulikuwa ukitamani siku nyimgi kuwa naye na hatimaye Mungu kakupa macho ya rohoni kumpata yeye.
Hapa wapo baadhi ya watu ambao si wakweli ambao wanafanya maigizo kutamka maneno kama haya huku wakitoa zawadi ili kuficha mambo yao huo ni usaliti na hapa nasema kuwa haifai….kama upo hivyo jirekebishe acha usaliti.
Mpenzi msomaji wa safu hii ya Hakunaga baada ya kuoina baadhi ya njia ambazo zinzweza kukusaidia kutojiingiza katika usaliti wa mapenzi na ndoa wiki ijayo tutaona nji kadhaa wanazoweza kuzitumia wanawake kuwa sumaku kwa wanaume wao.
Tchao…
Brother kalu

TACAIDS; WANAOSAMEHE HAWAPATI MAAMBUKIZI YA VVU




Afisa utafiti wa tume ya kudhibiti Ukimwi nchini(TACAIDS) Dr. Avoldia Mlokozi. 



Na Gordon Kalulunga, Mbeya



TUME ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS) imesema wanandoa na watu walio kwenye mahusiano, wakiwa na tabia ya kusameheana wanapokoseana, wanaweza kupunguza ongezeko la maambukizi ya VVU.



Hayo yalisemwa na afisa utafiti wa tume hiyo Dr. Avoldia Mlokozi alipozungumza na waandishi wa habari Jijini Mbeya katika mohojiano maalum.



‘’Ukitaka kuishi kwa usalama ni kuwa na msamaha kwa mwenzako badala ya kuchepuka kwenye ndoa kwa kisingizio cha kuudhiwa na mwenza wako’’ alisema Dr. Mlokozi.



Alisema katika kanda ya nyanda za juu kusnini magharibi, kiwango cha maambukizi ya VVU, mkoa wa Mbeya una asilimia 9, Rukwa 6.2 na Katavi ni 5.9 kiwanga ambacho ni kikubwa kuliko wastani wa taifa wa asilimia 5.1.



Alitanabaisha kuwa katika maambukizi hayo, wanawake ndiyo walioathirika zaidi kwa kuwa na maambukizi ya wastani wa asilimia 9.2 na wanaume asilimika 6.5 kwa takwimu za utafiti wa mwaka 2011-2012.



‘’Wanawake wanaopata zaidi ugonjwa huo ni wale wenye umri wa miaka kati ya 20 mpaka 30 kwasababu hao ndiyo wanakuwa kwenye mahusiano, kuolewa na kujifungua’’ alisema Dr. Mlokozi.



Aliongeza kwa kusema kwamba, tayari kuna mikakati ya elimu kwa lika hiyo ili kuweza kupunguza ushamiri wa maambukizi hayo ya VVU kwa wanawake.



Kuhusu mkoa wa Mbeya, alisema mkoa huo umeendelea kuathirika zaidi  na ugonjwa huo kutokana na mwingiliano wa watu kimaendeleo ikiwemo suala zima la uchumi ambapo baadhi ya wafanyabiashara na madereva wanaotumia barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam na kwenda Zimbabwe, Malawi, Zambia, Kongo na kwingineko kusini mwa Afrika, wanalala katika mkoa huo na kujiingiza katika mahusiano na baadhi hawatumii Kondomu.



‘’Nchi hizo zina maambukizi kuliko ya hapa nchini, hivyo pia ni moja ya sababu ya kuendelea kushamiri ugonjwa huo mkoani Mbeya na baadhi ya wanaume hawajafanyiwa tohara ambayo inasaidia kupunguza maambukizi kwa asilimia 60 na magonjwa ya zinaa’’ alisema Dr. Mlokozi.

MDAU ANATAFUTA ''MCHUMBA'' WA KUCHAT NAE

NIMECHECK STORY yako kwenye mtandao.

Mi nahitaji mchumba wa miaka 30-35 wa kuchat nae (rafiki wa kike) Naomba uniunganishe nae akipatikana kupitia blog yako.

My name is Johanes(40Yrs old) 0766 927620

Friday 25 October 2013

SIRI YA HERUFI YA MWANZO YA JINA LAKO

HERUFI A

Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa mambo makubwa, anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu mwenye tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda Mamlaka, na ana kiburi, na hasira. 

HERUFI B
wenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu, muaminifu, na hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake. 

HERUFI C
Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika, mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa wabunifu na wanaopenda mawasiliano.

HERUFI D
Mwenye jina linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa usawa, Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na wenye msimamo. 

HERUFI E
Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye roho nzuri ,yenye mapenzi na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu. 

HERUFI F
Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu mwenye mapenzi,huruma , roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi. 

HERUFI G
Mwenye jina linaloanzia na herufi G ni mtu mwenye mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho. Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. ni mtu mwenye hisia kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri wa kutoka kwa watu.

HERUFI H
Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni mtu mwenye ubunifu na nguvu katika biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na bidii zake. ni mwenye mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi. 

HERUFI I
Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni mtu mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu. Wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira za haraka. 

HERUFI J
Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni mtu mwenye matamanio,mkweli, mkarimu na muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa. Wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo. 

HERUFI K
 Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni mtu mwenye jeuri. mwenye msimamo thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. ni mtu asioridhika na hali ya kimaisha. 

HERUFI L
Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara. 

HERUFI M
Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye kujiamini sana, mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika. 

HERUFI N
Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu mwenye ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana. 

HERUFI O
Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra, mvumilivu na mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.

HERUFI P
Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu.

HERUFI Q
Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana.

HERUFI R 
Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma lakini ana hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda amani.

HERUFI S
Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa.

HERUFI T
Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa kiroho, anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika.

HERUFI U
Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na aliyekosa maamuzi.

HERUFI V
Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu Mchapakazi, wenye bidii na asie choka. Hata hivyo ni watu wasiotabirika.

HERUFI W
Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni mtu muwazi, wachangamfuu kupita kiasi na mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya. Ni watu wenye tamaa na hufanya mambo ya hatari.

HERUFI X 
Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni mtu asiyependa kuwekewa vizuizi katika kwenye anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu.

HERUFI Y (YASINTA)
Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye kupenda Uhuru na hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na husababishia kupoteza bahati katika maisha.

HERUFI Z
Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda matumaini na amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo.

Wednesday 23 October 2013

KONDOMU NA UKIMWI

  • KONDOMU ni kifaa/ zana iliyotengenezwa mahususi kuvalisha uume au kuwekwa ukeni wakati wa kujamiiana.Nazo hubana kutokana na umbile la uume au uke.

Kondomu hizi zipo za aina tofauti kutokana na muda na vipindi zilipotengenezwa, nazo ni kama ifuatavyo:-
  • Awamu ya I – zilizotengenezwa kwa mimea.
Hizi zilitengenezwa mahususi kama kinga dhidi ya maambukizo ya vimelea vya ugonjwa wa kaswende [ugonjwa wa kifaransa]

  • Awamu ya II – kutokana na utumbo wa kondoo.
Dr. Condom alifahamika kama mgunduzi wa kondomu hizi, naye alikuwa ni dakatari wa Mfalme Charles II. Alimshauri Mfalme kutumia kama kinga kutokana na magonjwa ya zinaa kutokana na tabia yake ya kuwa na wanawake wengi nje ya ndoa yake.

  • Awamu ya III – kutokana na mpira
Hizi zilitengenezwa kwa urahisi na kwa wingi na zikawa ndizo pekee zenye uwezo wa kudhibiti mimba hadi miaka ya 1960 vilipogunduliwa na vidonge vya majira.

JE KONDOMU NI SALAMA?
  • Tunaelezwa kuwa kondomu hutengenezwa kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba haziwezi kuruhusu kitu chochote kupita.

  • Lakini tafiti mbalimbali zilizofanyika zinaonyesha kuwa kondomu zaweza kuvuja kutokana na mazingira halisi ya utengenezaji wa latex.

  • Wengine wanadai kuwa ili kuzifanya imara, kondomu zimetengenezwa kwa kupishanisha pande mbili ili kuziba udhaifu wa kila upande.

  • Hata hivyo watengenezaji wanasahau kuwa mazingira ya matumizi ya kondomu katika ngono hayalingani na majaribio waliyofanya ya kujaza maji au hewa ili kupima kama maji na hewa vinapita.

  • Katika tendo la ngono ipo misuguano ya namna mbalimbali inayosababisha kubadilisha mazingira ya kondomu na kuidhoofisha.

  • Kutokana na tafiti hizo imefahamika kuwa kondomu hazina uwezo wa kuzuia mbegu za kiume kupenya wakati wote.

  • Upana wa kipenyo cha mbegu ni makroni 5 wakati upana wa kipenyo cha kirusi cha ukimwi ni makroni 0.1

  • Kwa maneno mengine mbegu ya kiume ni kubwa mara 50 ya kirusi cah ukimwi.

  • Vile vile tafiti zimeonyesha kuwa kondomu haina uwezo wa kuzuia maambukizo ya magonjwa ya zinaa vikiwemo virusi vya ukimwi kwa kiwango cha asilimia mia moja.

  • Hivyo tunaweza kusema kuwa, kondomu si salama kwa asilimia mia moja.

  • Kondomu zina kiwango cha kushindwa cha kati ya asilimia 10 na 15 na wengine wanasema hata asilimia 20.

  • Wasambazaji na wahamasishaji wa matumizi ya kondomu hawapendi kusikia ukweli huo na wanafanya jitihada kubwa ya kuficha ukweli huo.

  • Matangazo yatolewayo kupitia mabango ya barabarani, katika televisheni, radio na hata magazeti yanawarubuni watu yakiwaaminisha kuwa kondomu humkinga mtumiaji kwa kiwango cha asilimia 100%

  • Huko ni kukengeusha ukweli na kukiuka maadili ya kitaaluma.

  • Wengi kama sio wote wateteao matumizi ya kondomu hufanya hivyo kwa sababu ya maslahi ya kifedha na kibiashara.

  • Tukiongozwa na dhamiri safi, lazima tukiri ukweli uliopo na tuwaeleze watumiaji, ili tusijekuwa sababu ya kifo chao.

  • Kila kondmu inaposhindwa [itumikapo] kama kinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya ukimwi ] humaanisha kifo.


  •  
  1. Udhaifu wa kondomu
    1. Kiufundi
    2. Matumizi
    3. Kimazingira
 
  1. Udhaifu wa kiufundi
Wasambazaji wanatueleza kuwa kondomu zilizotoka kiwandani zikiwa na ubora unaotakiwa zikitumika wakati wote na kwa usahihi zina uwezo wa kukinga kwa kiwango hadi cha asilimia 97.

Zisipotumika vizuri zina kiwango cha kushindwa cha asilimia 14.

Kiwango cha kushindwa kwa kondomu kuzuia maambukizo ya magonjwa ya zinaa hutofautiana kutokana na aina ya magonjwa ya zinaa.

Kondomu zaweza kuzuia kwa kiwango fulani mambukizo ya magonjwa ya zinaa yanayosafiri kwa njia ya ute, lakini haziwezi kuzuia magonjwa ya zinaa yanayoambukizwa kwa mgusano wa mwili kama vile "herpes" na "human papillomavirus"; au magonjwa yanayoambukizwa kutokana na vidonda au malengelenge yaliyoko kwenye via vya uzazi kama vile kaswende.

Hali hiyo inatokana na:
  1. Watengenezaji wameruhusu udhaifu wa kiufundi kama zao la kiwandani lililotengenezwa na kazi ya mikono ya binadamu [acceptable quality limit] kwa kiwango Fulani kwa nchi mbalimbali. Mfano, Marekani kiwango kilichokubaliwa ni asilimia 99.6 kwa kutoruhusu kondomu kuvuja. Uingereza asilimia 97, Uholanzi asilimia 96. 5. Hivyo katika kila idadi ya kondomu itumikayo kwa wakati mmoja kuna kiwango cha kuvuja kati ya asilimia 0.4 (USA); 3% (Britania); 3.5% (Holland).

  2. Kondomu huzeeka
Kwa kadiri zisivyotumika kwa muda mrefu ndivyo hivyo zinaaendelea kuzeeka. Kwa hiyo mtumiaji kondomu wa miaka 3 au 4 baada ya kondomu hiyo kutengenezwa yumo katika hatari zaidi kuliko anayetumia kondomu mara tu baada ya kutoka kiwandani.

Utafiti mmoja umeonyesha kuwa kiwango cha kupasuka kwa kondomu kiliongezeka kutoka 3.6% kwa kondomu mpya hadi 18.6% kwa kondomu zilizotumika miaka kadhaa baadaye.
  1. Kondomu hupasuka. Kiwango cha kupasuka hutegemea aina ya kilainisho kilichotumika na aina ya kondomu. Kwa mujibu wa tafiti 15 zilizofanywa na "Contraceptive Technology" yalionyesha kuwa katika kondomu 25,184 zilizotumika 4.64% zilipasuka.

  2. Ingawaje kondomu za latex zinaonekana kuwa na kiwango kidogo sana cha kupitisha virusi vya ukimwi, hatari kubwa ya matumizi yake imo katika uwezekano wa kondomu kupasuka, kuteleza na kuteleza.

Kwa hiyo hata kama ni virusi vichache tu vinaweza kupenya, kiwango cha maambukizo kitakuwa kikubwa kadiri kondomu zinavyosambazwa kwa wingi na kadiri watu wanavyojihusisha na vitendo vya ngono wakiamini katika matumizi ya kondomu.

b. Udhaifu katika matumizi
  1. Matumizi mabaya: yaani kutovaa vizuri, kuvaa nje ndani, aina ya ngono, urefu wa muda wa ngono, pia kutokana na uelewa mdogo hasa kwa wasojua kusoma na kuandika na wale wakaao mbali na mijini.

  2. Kuteleza na kuvulika kutokana na hali ya uume kuwa mdindifu au la; upana au wembamba; mrefu au mfupi. Pia kutokana na tendo la ngono na hali ya mtumiaji na mazingira ya matumizi. Kutokana na umri wa mtumiaji, kama ni mtoto, kijana, mtu mzima au mzee.
  3.  
  4. Kutumia kondomu ambazo muda wake umepita. Mfano wanaotumia gizani , katika hali ya ulevi, kutokujua kusoma, kuchunguza na kugundua kama muda wake umepita.
  5.  
  • Mazingira ya kingono yakishawekwa, watu     wanatawaliwa na mihemuko ya juu ya ngono kiasi kwamba hawawezi kuchunguza tarehe ya ukomo wa matumizi ya kondomu.

  • Ingawa watengenezaji wanashauri kutotumia kondomu iliyobadilika rangi au iliyokauka, tabia za watumiaji hazina nafasi ya kuzingatia ushauri huo.
  •  
  1.  Lengo la mtumiaji laweza kusababisha matumizi kuwa mabaya. Mtu mwenye virusi vya ukimwi, anajiwekea lengo kwamba hataki kufa peke yake, atafanya jitihada za kutokutumia vizuri ili mwenzake [ambaye anaamini hajaambukizwa] aweze kuambukizwa ili, "nisife peke yangu".

Vilevile katika siku hizi za dawa za kupunguza makali ya kuzaliana virusi vya ukimwi, mtu anaweza kuonekana mwenye afya nzuri kabisa, na anaweza kumshawishi mwenzake kuachana na kondomu kwa vile "wanaaminiana".

Kwa hiyo mambukizi yanaweza kuwa makubwa kutokana na kutowadhibiti wale waliokwisha ambukizwa.
  1. udhaifu wa kimazingira

Huu unatokana na hali zifuatazo:-
  • kibinadamu
  • kimaumbile
i. Kibinadamu
Udhaifu wa kondomu waweza kusababishwa na usafirishwaji, yaani muda unaotumika kusafiri kutoka sehemu zinapotengenezwa hadi mahali zinapotumika;
 
ii. Kimaumbile
Vyombo vya usafirishaji  na usalama wa vyombo hivyo;

Kondomu zinazosafirishwa katika meli, zikiwa baharini kwa miezi kadhaa kabla hazijafika katika nchi lengwa na katika hali ya joto ndani ya makontena zinakuwa na kiwango hafifu katika ubora wake.

Udhaifu wa sehemu ya kuhifadhi kondomu pamoja na vyombo vya kuhifadhia.
Search Site
source. Human Life International

UZAZI WA MPANGO KWA NJIA YA ASILI

“BILLINGS OVULATION METHOD”

Ili kujifunza njia hii vizuri, ni vyema kuvifahamu vizuri viungo vya uzazi vya mwanamke na jinsi vinavyofanya kazi.

Viungo vya uzazi vya kike:
  • Hypothalamus
  • Glandi ya Pituitary
  • Tumbo la uzazi
  • Ngozi nyororo
  • Mlango wa tumbo la uzazi
  • Uke
  • Mirija miwili
  • Vifuko viwili vya vijiyai
  • Vijifuko vya vijiyai na vijiyai

Msichana anazaliwa na vijiyai vingi, lakini vyote ni vichanga. Wakati wa kubalehe viungo hivi vinaanza kushirikiana na kuwa na mahusiano kama ifuatavyo:-
  1. Sehemu ya ubongo iitwayo Hypothalamus, inaamsha Pituitary Gland                 
kutengeneza chachu mbili:

 (1) Follicle Stimulating Hormone- kazi yake ni kuamsha kijifuko cha kijiyai na kijiyai
        kukua.   

  (2) Luteinising Hormone- kazi yake ni kupasua kijifuko cha kijiyai       
       na kukiondoa kijiyai baada ya kuiva.
   
  1. Wakati wa kukua kijifuko kinatengeneza chachu ya Estrogen.
               Estrogen ina kazi mbili:
  1. Kuamsha ngozi nyororo kukua
  2. Kuamsha vikunjo vya mlango wa tumbo la uzazi vya L, S, P kutengeneza ute wa kuvutika na kuteleza, yaani ute wa uzazi. Wanawake wengine wanaona furaha wakati Estrogen inapofanya kazi.
  3.    
  4. Baada ya muda kijiyai huiva na LH inapasua kijifuko na kukitoa
kijiyai.Hii huitwa Ovulation:- kuchopoka kwa kijiyai.
Kijiyai kinapokelewa katika mrija, kinaishi hapa kwa siku moja tu (masaa 24), na kinakufa hapohapo na kuyeyuka hapohapo.
  1. Mara baada ya Ovulation kijifuko kinabadilisha:-
    1. Kazi yake: Inatengeneza chachu ya Progesterone na kuongeza tena Estrogen.
    2. Jina lake huitwa sasa Corpus Luteum.
    3. Rangi yake: Kuwa manjano na inafanya kazi kwa muda wa siku 11-16.
 
  1. Progesteron ina kazi tano:-
    1. Inasimamisha Pituitary Gland kutengeneza F S H na L H, ili kijiyai kingine kisiive sasa.
    2. Inarefusha mishipa ya damu ya ngozi nyororo na kuikunja, ili binadamu mpya apate chakula na oxygen ya kutosha akizama hapa.
    3. Inapandisha joto la mwili kidogo kiasi cha 0.°C - O.6°C
    4. Inaamsha vikunjo vya chini vya mlango wa tumbo la uzazi kutengeneza ute mzito sana, ute wa (G) ambao haupitishi mbegu za bwana na kufunga mlango wa tumbo la uzazi mpaka hedhi inapoanza au mpaka kuzaa.
    5. Inaamsha “Pockets of Shaw” kutengeneza manganizi kwa kukausha ute wa uzazi.
         Angalizo: Kwa wanawake wengine wanaona moyo mzito kidogo
                          Progesteron inapofanya kazi.

  1. Kama mama hakupata mimba, Corpus Luteum inaacha kazi yake baada ya siku 11-16 na chachu za Estrogen na Progesteron zinapungua. Hapo ngozi nyororo inatoka pamoja na damu na joto la mwili linashuka tena. Hii huitwa hedhi.

MLANGO WA TUMBO LA UZAZI, VIKUNJO VYAKE NA AINA YA UTE

A.      Katika mlango wa tumbo kuna vikunjo mbalimbali-
  • vikunjo vya L, S, na P vinatengeneza ute wa uzazi Estrogen ikizidi.
  • vikunjo vya G vinatengeneza ute usio na uzazi Progesteron ikizidi
  •  
  1. Ute wa G kazi yake ni :-
Kufunga mlango wa tumbo la uzazi. Mbegu za baba na vijidudu vya magonjwa haviwezi kupita. Ute wa G hauna uzazi.
 
  1. Ute wa L kazi yake ni:-
  2.  
  • Kuchuja mbegu dhaifu 400,000,000→200.
  • Kufungia mbegu zenye nguvu katika vikunjo vya S. Ute wa L una uzazi.
  •    
  1. Ute wa S kazi yake ni:-
  • Kulisha mbegu za baba, zinaishi siku 3-5. Katika mazingira yasiyo na uzazi zinakufa kabla ya nusu saa.
  • Ute wa S unaziwezesha mbegu kuingia katika tumbo la uzazi.Ute wa S una uzazi.
  •  
  1. Ute wa P kazi yake ni:-
  • Kuyeyusha ute wa G na kufungua mlango wa tumbo la uzazi.
  • Pamoja na Enzyms wa Z-granula, huyeyusha ute wa L na kufungua vikunjo vya S ili mbegu ziweze kutoka na kuingia katika tumbo la uzazi na kufuata kijiyai.
  • Huzisukuma mbegu ndani.
  • Kuchuja mbegu za baba.Ute wa P una uzazi.
  •  
  1. Ute wa F kazi yake:- Haijulikani.
        

MIANDAMO

1. AINISHO: Mwandamo ni muda kutoka siku ya kwanza ya hedhi mpaka
    siku ya kwanza ya hedhi inayofuata.

2. Mabadiliko mbalimbali katika mwandamo: damu, ukavu, ute mzito,
    ute wa kuteleza, ukavu tena n.k

3. Aina ya miandamo.
(1) Mwandamo wa wastani, siku 25-34
(2) Mwandamo mfupi, siku 18-24
(3) Mwandamo mrefu, siku 35-50 au zaidi
(4) Mwandamo bila utaratibu.


*Hakuna sababu ya kurekebisha mwandamo, ni maumbile yake.
  Wasitumie dawa ya chachu bandia, zina madhara mengi, pia zinaleta utasa.

SIKU YA KIJIYAI KUCHOPOKA

Umuhimu wa kilele ni kwamba kijiyai kinachopoka hapa, yaani siku ya kilele yenyewe, au siku moja baada ya kilele, au siku ya pili baada ya kilele.

*Kama kawaida kijiyai kimoja tu kinachopoka katika mwandamo mmoja. Lakini inaweza kutokea kwamba vijiyai viwili au vitatu vinachopoka. Lakini vyote vinachopoka siku moja tu, yaani katika masaa 24. Vijiyai vyote vinaishi masaa 24 tu. Hakuna kijiyai kinachoiva tena mpaka mwandamo unaofuata.


DALILI ZA KUCHOPOKA KIJIYAI                       
  1. Kilele.
  2. Mdomo wa uke unavimba upande kijiyai kinapoiva.
  3. Tezi kwenye nyonga inavimba upande kijiyai kinapoiva.


KANUNI ZA KUPUMZIKA KUZAA

  1. Kanuni ya kutogusana
Kuacha tendo la ndoa kabisa wakati wa siku zote za uzazi, yaani:
  • bwana asimwage mbegu nje
  • wala mapajani
  • wala kinenani
  • wala kugusana viungo vya uzazi nje, kwa sababu tone dogo la shahawa linaweza kutoka kabla ya mshushio au mshindo na mbegu zinaweza kuingia katika ute wa uzazi uliopo nje na kuogelea katika mifereji ya ute wa uzazi mpaka ukeni na kusababisha mimba.
  • wala kutumia dawa za majira
  • wala kutumia kondomu siku za uzazi.

  1. Kanuni za mapema
    1. kuacha tendo la ndoa wakati wa hedhi.
    2. kuacha tendo la ndoa wakati wa damu kidogo na siku 3 baadaye.
    3. kuacha tendo la ndoa wakati wa ute wa uzazi na siku 3 badaye.
    4. kufanya tendo la ndoa wakati wa siku zisizo na uzazi, ukavu, ute mzito usiobadilika, aina ya majimaji yasiyobadilika jioni tu, si kesho yake.

?Jioni tu: kwa sababu mama ana hakika kama ana ute wa  uzazi au siyo.

?Si kesho yake: Mama hawezi kutofautisha kama ute ni wa
                            mume tu au kama mwenyewe ameanza pia
                            kupata ute wa uzazi.

  1. Kanuni ya kilele
Kuacha tendo la ndoa siku ya kilele na siku tatu baada ya kilele. Kuanzia siku ya nne baada ya kilele tendo la ndoa linawezekana siku na saa yoyote mpaka mwisho wa mwandamo.


FAIDA ZA KUPUMZIKA/ KUACHA TENDO LA NDOA KWA MUDA

  1. Mke apate nafasi ya kujitambua wakati wa kujifunza BOM.
     Kujichunguza ili kuelewa mtiririko wa Ishara zake za uzazi kwa muda    
     wa wiki 2-4.

  1. Mume apate nafasi ya kujenga afya yake wakati wa kujifunza BOM.

     3.  Utaratibu katika ndoa: Kujishinda kunasaidia Kujitawala, na kunaleta      
ukomavu wa akili, mwili na roho, mume anakuwa mtu mwenye maamuzi ya busara.

  1. Uhusiano kati ya mume na mke unaboreshwa, kwa sababu wanaongea mara kwa mara kuhusu siku ya uzazi na zisizo na uzazi.

  2. Inazidisha heshima, upendo na amani. Baba anamjali mkewe,
           wanaheshimiana, mke hawi chombo cha mume kujifurahisha.
     Wanafurahishana katika umoja wa miili.          
  1. Kunaimarisha ndoa na familia. Kwa sababu kunaamsha mapendo ya dhati ambayo yanapata nafasi ya kuonekana katika matendo mengine. Kama wanandoa wanaonyesha mabadiliko ya uwajibikaji katika maisha yao na hivyo watoto wanaiga mifano bora ya maisha ya wazazi. Wanaonyesha upendo, upendo huu siyo kuufunga katika tendo la ndoa pekee.

  2. Kunaimarisha Jamii na Taifa kwa ujumla. Kwa sababu wanandoa wanakuwa na tabia ya kuwajibika kwa ajili ya mtu mwingine na kushinda ubinafsi katika tendo la ndoa. Kunajionyesha pia hata sehemu za kazi na kwa kiasi kikubwa na chanzo safi cha kushinda tabia ya kuomba na kupokea rushwa na hivyo Taifa linakuwa la watu safi.

Monday 21 October 2013

WANAUME WANAPENDA KUOA WANAWAKE WENYE TABIA HIZI

Hakunaga na Brother Kalu


WAPENZI wasomaji wa safu hii niwashukuru sana hasa wadau wa Sumbawanga wakiwemo wanafunzi wa ST. Maurus Chemichemi ambao mliamua kuniita kwa ajili ya kufahamiana, hakika mlionesha moyo mkubwa wa upendo na haja ya kutaka kujua mambo mengi kuhusu mahusiano ingawa muda haukutosha lakini ibaki historia kuwa tulionana.

Jana tuliona dalili za mwanamke ama mazingira yanayomfanya kupenda na kujisikia kufanya mapenzi, wiki hii kama nilivyowajuza tuone wanaume wanapenda kuoa wanawake wenye tabia zipi.

Mtu anaweza kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na wakati mwingine kwasababu ya kukidhi tamaa ya ngono kisha akabaini kuwa anaona mvuto mkubwa kwa mpenzi huyo. Upande mmoja ama pande zote zaweza kudhani kuwa mvuto huo ndiyo dalili za kuwa na mapenzi ya kudumu jambo ambalo ni kosa na athari zake huonekana baadae.

Sasa tukijite kwenye kitovu cha mada tajwa hapo juu ambapo wanaume wengi wanaojua athari za kukurupuka kuoa wanapofikia hamu ya kuoa si kwamba wanakurupuka bali huwachukua muda mrefu kuchunguza hata kama wataona wanawake wazuri wa sura.

Hapa ni kipindi kigumu sana kwa wanaume na wanawake wengi hujidanganya na kufikiri kuwa kitu kinachoweza kuwashawishi wanaume kuwa nao kwa ndoa ni kujiremba kupindukia hivyo wengi huishia kupoteza muda na gharama kubwa na kusahau kuwa kuolewa ni zaidi ya uzuri wa sura na kujiremba.

Hapo awali mwanamke mwenye umbo zuri na sura nzuri alikuwa na asilimia zaidi ya 90 za kuolewa lakini hali imebadilika ambapo wanawake wenye sura nzuri na maumbo mazuri wamekuwa ni wanawake wa kustarehesha wanaume na kupungukiwa sifa za kuolewa ambapo wanaume wengi wanasema kuwa wakiwaoa ni wasumbufu na wana viburi kutokana na kutongozwa na wanaume wengi hivyo kujiona kuwa soko lake ni kubwa hata akiachika.

1.Mapenzi Mema yenye faraja si makwazo
Lengo kubwa la mwanaune kuoa ni kupata mapenzi ya kweli na faraja kutoka kwa mkewe na hatimaye kupata watoto ambao wataongeza faraja katika familia na hatimaye kujivunia katika jamii mnayoishi.

Kumekuwa na tabia za wanawake wengi kupenda sana matukio kwamfano wengi wao wanapenda kuonekana wameolewa lakini maisha ya ndoa hawayataki na hawa tunawaita wanawake wazugaji na baadhi wanapenda pesa za mwanaume ama kuonekana yupo na Fulani.

Wengi wao hawajui kuwa maisha yanabadilika waweza kuwa nacho leo na kesho ukakosa na kusahau kuwa maisha ya ndoa kila uchwapo yanatakiwa kutawaliwa na upendo.

Niwakumbushe wanawake mambo walau matatu yanayoweza kuboresha mahusiano na maisha ya ndoa ambayo ni neno Samahani, pole na Asante yakizingatia hayo yatakusaidieni.

2. Mwanamke mwenye tabia Njema
Mwanamke ukiwa na tabia njema kwa kujitambua kuwa wewe ni mwanamke tayrai unakuwa umejiweka katika asilimia kubwa ya kuolewa na mwanaume wa ukweli mwenye uhitaji wa kuwa na mke maana tabia njema waswahili wanasema ni silaha.

Hakuna asiyejua umuhimu wa silaha na ndiyo maana wenzetu wazungu walio wengi wanathamini sana wapisgi na walinzi wao maana hao wameshika asilimia Fulani za uhai wao.

Linapokuja suala la kuoa hakuna mtu anayeuliza kuwa mwanamke anayetaka kuolewa ana kimo gani ama umbile likoje bali kitu cha kwanza kuuliza ni tabia watu wanaulizana ama kuambia kuwa je unaijua tabia yake? Na je unaona mtawezana na huyo mbona chakaramu huyo? Huku wengine wakisema aaaaaa.. pale umepata mke ana tabia nzuri sana na anaheshimu mkubwa na mdogo na anamisimamo.

Wapo wanaume walikurupuka kuona wanawake wenye sura na maumbile mazuri lakini baada ya siku chache kilichotokea ni machafuko makubwa na hatimaye ndoa zikavunjika na hawatamani tena hata kuwa na mahusiano ya kawaida na wanawake warembo.

3. Wenye kupenda kutoa ushauri wa kimaendeleo.
Kuna tabia mbili ambazo wanaume wanapenda kuziona kwa wanawake ambao wanatamani kuwaoa. Wanaume wengi kwa sasa hawapendi kuoa mwanamke ambaye hana kazi na vinginevyo mwanamke huyo atakuwa na mawazo chanya ya kimaendeleo.

Mwanamke mwenye fikra za kumshauri mwanaume wake masuala ya kimaendeleo na mwenye kujituma bila manug’uniko na kutoa lawama hata kwa vitu vidogo alivyotendewa na mpenzi wake ana nafasi kubwa ya kuolewa kuliko ambaye ana ajira yake kwasababu mawazo ni dira ya kila jambo.

Hapa sizungumzii mwanamke ambaye anapenda kunyoosha miguu nyumbani na kuagiza ama kupanga mambo ambayo anataka afanyiwe na mtu mwingine, la hasha bali nazungumzia mwanamke ambaye anapenda kumshirikisha mwenzi wake jambo ambalo wanaweza kulifanya kwa pamoja ama kupanga kwa ajili ya maendeleo yao na jamii inayowazunguka ikiwemo kutoa misaada kwa wahitaji ama kutembelea wagonjwa Hospitalini.

Mwanaume hapendi kuwa na mwanamke ambaye anapenda makuu, si unajua kuna wanawake si vijijini wala mijini wao makuu kwao ndo maisha, na hapa nitoe dawa inayoitwa limbwata, limbwata linalotakiwa hapa ni kwamba wanaume kama watoto wanapenda sana kunyenyekewa na hilo ni limbwata baaab kubwa hivyo mwanamke haupaswi kupenda makuu ni moja ya dalili inayokukosesha kuolewa ama kuaminika katika jamii unayoishi na kama upo kwenye ndoa tambua mwanaume wako anaporudi nyumbani anaona kama anaenda Rumande.

4. Wanawake wavumilivu
Wapo wanawake ambao si wavumilivu hata chembe katika maisha, wao akili zao zimeganda kuwa maisha yanasonga mbele bila kujua kuwa kuna wakati wa majaribu lakini kila jaribu lina mlango wa kutokea maana katika maisha ama katika mahusiano kuna matatizo ya kiafya na hata kukwama kabisa kifedha kwa mwanaume ambapo wengi wetu husfikia hatua ya kusinyaa ni kutokana na mawazo.

Matatizo ya kiafya au ukosefu wa fedha ni moja ya wakati wa kipimo kwa kutambua mwanamke mvumilivu ama matatizo mengine si tumeshuhudia wengi wakiwatoroka waume zao na kuachanana wapenzi wao kisa matatizo jambo ambalo kwa mwanamke wa namna hiyo hujidhihilisha kuwa hana sifa ya kuwa mke wa Mtu.

Baada ya kuona baadhi ya tabia ambazo wanaume wengi wanapenda wazione kwa wanawake wanaotaka kuwaoa, wiki ijayo tutaona ni vitu gani muhimu vinavyotakiwa kuwepo kabla ya kufanya mapenzi.

Teta nami kupitia
0655 440749 

Sunday 20 October 2013

DALILI TISA ZINAZOMSHAWISHI NA KUMPA RAHA MWANAMKE KUFANYA NGONO

 Hakunaga na Brother Kalu

Nawashukuru wote tulioweza kuwasiliana mkipongeza safu hii kupitia simu zenu za viganjani na baadhi tukishauriana ili kuweka sawa na kusuluhisha baadhi ya migogoro ya kimahusiano ambapo leo tuzitazame dalili za mwanamke anapotaka ngono.

Kwanza kabisa nikujulishe kuwa kitaalam mwanaume huwa anawaza ngono kila baada ya sekunde sita huku akiwa za mahala pa kufanyia tendo hilo wakati mwanamke huwaza ngono kila baada ya sekunde tisa na akikubali kuvua nguo ni lazima awe na sababu za msingi.

‘’Mimi sijisikii kufanya mapenzi’’ hii ni moja kati ya kauli ambazo wanaume huambiwa na ukisikia hivyo ujue si peke yako unayeambiwa hivyo na hii ni kauli inayolalamikiwa sana na wanaume wengi ambapo baadhi yao wamediriki hata kuchepuka wakidhani wenzi wao wamewachoka, hapana....na makala haya inakufungua.

Broher Kalu nakuambia kuwa, Wanawake wanapagawa na huhitaji kufanya mapenzi kuliko wanaume wengi wanavyodhani na ukijua mazingira hayo walai hautamwacha mwanamke wako naye hatatamani mwingine kwasababu wanawake wanajieleza wazi kuwa katika mazingira nitakayoyataja hapa chini yakifuatwa wanajisikia raha mno…

1.      Mfurahishe
Hali yeyote ya furaha kupita kiasi inamfanya mwanamke kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kufanya mapenzi bila kizuizi chochote.

2.     Baada ya kuzozana
Kugombana ninakozungumzia hapa ni kule kwa pande mbili mnakwazana na baadaye kila upande ukatoa dukuduku zake hata kama kwa kufikishana kwa wakubwa kwa nia ya kupata muhafaka na baada ya hapo hakuna kitu kizuri cha kubadilisha upepo huo zaidi ya kukumbatiana, kubusiana kwa huba huku mkiziamsha hisia zenu.

Ukiona hata kama mwanamke wako analia au ameghafirika kwelikweli, mwache anyamaze au mnyamazishe huku ukimbembeleza hata kumfuta machozi kisha …….hapo tatizo linaisha na wakati huo wote kwa pamoja mtafurahia tendo hilo.

3.     Siku ya 14 (Heat Period)
Wataalam husema kuwa hiki ni kipindi cha joto kwa mwanamke, ni kipindi cha aina yake katika mahusiano ambapo mwanamke anakuwa na hisia nyingi wakati mayai yanapotungwa.

Hivyo zikiwa zimepita wiki tatu baada ya kumaliza Afya yake ya ‘’uchinjaji kisha damu kukauka’’ wakati huu ni muhafaka kufanya mapenzi na hata kama mwanaume ni mbishi kiasi gani au umechoka mwanamke atakuamsha na kukutega na mara nyingine atakueleza kuwa anataka.

4.     Mapenzi ya Mbali.
Mapenzi ya mbali yanaweza kuwafanya mkawa na maisha yasiyokuwa na migogoro ya mara kwa mara huku kila mmoja akiwa anamtamani mwenzake na kitu pekee kwa wakati huu wa utandawazi kinachoweza kuwaunganisha zaidi ni simu na internet.

Mkikutana siku hiyo kila mmoja anamtamani mwenzake na kama ni asubuhi mtaona siku haiendi haraka hasa kwa wale wenye familia na kama mtakuwa wawili katika chumba ama nyumba hiyo aaaaaaahhhhh hiyo niwape hongera kwasababu hamtakawia hata sebuleni.......

5.     Wivu
Ninachozungumzia hapa si ule wivu wa kijinga bali nazungumzia wivu wa mwanamke anayejitambua na kujiamini kuwa anamtii, kumnyenyekea na kumshauri kwa hekima mwanaume wake lakini anapata wivu anapoona mwanaume huyo yupo na mwanamke mwingine hata kama si katika mahusiano. Si unajua kila mtu ana moyo wa nyama? Hasa ukipenda, weeeeeee acha tu!

Mwanamke anapoona mwanaume wake ananyemelewa na mwanamke mwingine na kumshawishi kimapenzi huona wivu sana na wanawake wanaojitambua badala ya kufoka huamua kuwaonyeshea wanaume wao kitandani kwa kuwapa mapenzi motomoto huku wakionyesha stahili na kuonyesha kujiamini kuwa ni wazuri kila upande yaani sura, maumbile na hata kitandani kuliko wale wanaomnyemelea.

Hapa siruhusu wanaume kuwa vicheche ama kuambatana na wanawake wengine bila sababu eti tu unataka mwanamke wako akuonee wivu hapana hii ni mbinu ya kuotea maana kumrusha roho mtoto wa mwanaume mwenzako si vema.

6.     Mwanamke kujinyima
Kadri mwanamke anavyozidi kukaa muda mrefu bila kufanya usodoma na ugomora, ndivyo anazidi kupata ashki ‘’Nyege’’ na mwanaume unapompata mwanamke aliyekaa muda mrefu hakika utafaidi na yeye pia atakuweka kwenye historia maana atajisikia raha sana baada ya tendo hilo.

Na mwanamke wa namna hii haitoshi kuwa mmefanya tendo la ndoa siku moja huyu atahitaji walau siku mbili vinginevyo ukimwacha atachepuka ingawa ni wachache wanaoamua kufa kisabuni na kuamua kutumia maji ya moto kujikanda.

7.     Mawazo
Mwanamke ambaye amekuwa na mawazo kwa muda mrefu akihitaji faraja na akakosa hatimaye Mungu na malaika wake wakamwangazia nuru na kujikuta mikononi mwa mwanaume anayeweza kumpa mapenzi yatakayomfariji hakika mwanamke hufurahia tendo hilo ambalo anahisi linakata kiu yake na kushusha pumzi.

8.     Mbunifu wa Mazingira
Wanaume wengi wanawanyima uhuru wa mazingira wanawake zao huku wakihoji ‘’ameyapata wapi haya’’ nakushindwa kujua kuwa huo ni moja ya mtego wa kutaka mapenzi.

Mwanamke anaweza kukutaka mfanye mapenzi jikoni, bafuni, sebuleni kwenye kiti au popote pale na kama amekupagawisha vizuri katika penzi la jikoni kuna siku mnaweza kujikuta mkiacha chakula kikiungulia huku nyie mkiwa mnatoa jasho la Afya na hapo mwanamke atafurahi kwasababu mtego wake wa kwale haujanasa chui.

9.     Muziki na Kinywaji
Kucheza muziki na wengine wale ambao wanapata kidogo kinywaji ni moja ya mambo ambayo yanasisimua mwili na kuamsha hisia za mahaba kwa mwanamke.

Hapa kwa mwanaume unaweza kumchukua mwanamke wako na kwenda naye kwenye kumbi za Muziki kwa Sumbawanga wakati ule sijui kwa sasa kulikuwa na ukumbi wa Upendo View, Mbeya zipo nyingi ikiwemo Mbeya Carnival, Pamodz wakati Dar es Salaam kumbi ni bwerere, Tanga bado sijazungumia..... 

Wakati mnacheza jaribu kugusana ama kupapasana taratibu hapo mwanamke yeyote mradi akikubali kupapaswa, mambo yanakuwa si mambo.

Vipi unataka niendelee kutoa semina?.....hapana kwa leo tuishie hapa lakini wakati tukitafakari kuhusu dalili hizo za mwanamke ama mazingira yanayomfanya kupenda na kujisikia kufanya mapenzi, je mwanamke unafikiri kuwa mjuzi wa staili za mapenzi kunamshawishi mwanaume kukuoa ama kuendelea kuwa na wewe?

Tunatoa mafunzo na mbinu mbalimbali za kimahusiano kwa Tsh.10,000/= kupitia email au simu za viganjani na wale wanaohitaji kusuluhish migogoro yao tuiteni.

Teta nami kupitia


0655 440749 

Saturday 12 October 2013

ZISOME HIZI KUIMARISHA MAHUSIANO YAKO NA MWENZA WAKO


Watu Wengi Ambao Wako Kwenye Uhusiano Wanalalamika Kuwa Wenzi Wao Hawawaoneshi Upendo Kama Ilivyokuwa Siku Za Mwanzo Za Uhusiano Wao. Wanaeleza Kuwa Wanaona Uhusiano Wao Unalegalega Na Mapenzi Yanapungua Taratibu Kama Barafu Iyeyukavyo Juani.

Ili Kuepuka Yote Haya, Hauna Budi Kujifunza Njia Za Kuwasha Upya Moto Wa Upendo Kila Wakati Kwa Kuongeza Ukaribu (Intimacy) Kati Yako Na Mwenzako.

Zifuatazo Ni Mbinu Zitakazokusaidia:

1. Kucheka Pamoja

Kicheko Ni Mlango Wa Ukaribu, Kama Mwaweza Kucheka Pamoja Basi Mwaweza Kulia Pamoja, Na Hapa Mwaweza Kuaminiana Zaidi Katika Kuwasiliana Hisia Zenu, Kama Waweza Kuitofuta Furaha Katika Kila Kitu Basi Unaweza Kupenya Katika Vyote. 

Usiwe Mgumu Na Mwenye Msimamo Mkali Katika Kila Kitu. 

 Jifunze Kujizuia Pale Unapoanza Kuelekea Kwenye Kukasirika Na Badala Yake Tumia Kucheka Kama Mlango Wa Kutokea. Kama Utaanza Kujizoeza Hivi Ukiwa Nyumbani, Taratibu Utaweza Ukiwa Ofisini Na Hata Kwingine Kokote.





2. Jifunzeni Kutiana Moyo

Kila Mmoja Awe Msaada Na Tegemeo Kwa Mwenzake. Jifunze Kumtia Moyo Na Kumwezesha Mwenzako. Sikiliza Na Kufuatilia Vile Mwenzako Afanyavyo Au Apendavyo.

Onyesha Heshima Katika Vitu Hivyo Pia. Kila Upatapo Nafasi Mpongeze Mbele Za Watu Au Hata Unapokua Nae Peke Yenu. Mjenge Mwenzako Mbele Ya  wengine Na Kubali Pongezi Zote Za Mafanikio Yenu Zimwendee Yeye. Mruhusu Mpenzi Wako Ajue Kuwa Una Mkubali Katika Kila Afanyalo. Zaidi Tunavyo Wainua Wapenzi Wetu Ndivyo Wanavyotuthamini Na Kutunyanyua Na Sisi Pia.

3. Jifunzeni Kupenda Kugusana

Nguvu Ya Mguso Wa Ukaribu Kamwe Haiwezi Kulinganishwa Na Chochote. Lazima Mjifunze Kujenga Tabia Ya Kugusana Mara Mpatapo Nafasi Sio Tu Mnapokuwa Mmelala. Kugusana Huku Ni Pamoja Na Kushikana Mkono Mkiongea Au Mkitembea, Kukumbatia Bega, Kugusa Au Kuchezea Nyewele Za Mwenzako Na Njia Nyingine Zozote Za Kuonyesha Ukaribu Kimwili. Wengi Wetu Huweza Kufanya Haya Kidogo Tunapokuwa Peke Yetu Na Kamwe Sio Mbele Ya Watu, Je, Ni Aibu, Nidhamu Mbaya? Dhambi?
Kugusana Ndiyo Mwanzo Wa Kuamsha Hisia Za Kuhitajiana, (Hebu Jiulize Kisirisiri, Lini Uligusana Na Mwenzako Nje Ya Chumba?). Kumgusa Umpendaye Hukuzuia Kutowaza Kumgusa Yeyote Katika Ulimwengu Uliojaa Wengi Walio Wapweke.

Mguso Huu Wa Upendo Haumaanishi Mguso Wa Tendo La Ndoa, Ingawa Pia Ni Vyema Kujifunza Kuijenga Lugha Ya Mguso Wa Tendo La Ndoa Katika Uhusiano Wenu.



 4. Zungumzeni Hisia Zenu

Kati Ya Vikwazo Vikubwa Katika Ustawi Wa Uhusiano Mengi Hususan Ya Wanandoa Ni Kutokuwepo Kwa Majadiliano. Lazima Wapenzi Wajifunze Kuzungumza Kuhusu Hisia Zao. Kama Vile Maisha Yasivyo Na Ukamilifu, Uhusiano Na Hata Ndoa Pia Hazina Ukamilifu. Mpenzi Wako Hayuko Kamili Na Wala Wewe Pia Siyo Mkamilifu. Jifunze Kuzungumza Na Umpendaye Jinsi Unavyojisikia Na Nini Kinachokusumbua. Kuendelea Na Migogoro Isiyosuluhishwa Husababisha Moyo Kuwa Baridi Juu Ya Mwenzako. Jiwekeeni Muda Kila Wiki Wa Kutoka Ili Kuzungumza Mambo Yenu. Mwambie Umpendaye Yapi Yanayojiri Kila Siku Na Zipi Ni Changamoto Zako Mkiweza Kujifunza Kuwekeza Katika Muda Wa Kuwa Pamoja Taratibu Hata Muda Wenu Wa Maongezi Ya Simu Utaongezeka.

5. Samehe Na Kubali Kusamehewa

Kamwe Tusiache Maumivu Na Machungu Yatawale Uhusiano Wetu. Lazima Tujifunze Kuwasamehe Tuwapendao Na Kujisamehe Sisi Pia. Kutofautiana Katika Uhusiano Kupo Sana, Na Lazima Tuwape Tuwapendao Nafasi Ya Kuelezea Vile Vinavyowaudhi Dhidi Yetu. Kila Hisia Za Mmoja Wetu Zina Umuhimu. Huwezi Kujiona Vile Ulivyo, Mruhusu Mwenzako Akwambie Yanayomuumiza Na Msameheane.

6. Linda Mwonekano Wa Mpenzi Wako

Mara Nyingi Hatari Hii Hutokea Tunapokuwa Katika Mizunguko Ya Huku Na Huko. Ukaribu Na Mpenzi Wako Hauendelezwi Tu Bali Unalindwa. Mwonekano Wetu Lazima Uwe Halisi Na Siyo Bandia . Vile Tunavyoviona Katika Tamthiliya Na Filamu Siyo Ukaribu Ulio Halisi. Kama Tunataka Tuonekane Sawa Na Vile Tunavyowaona Wengine Wanavyopendana Basi Tunakosea Na Kujizuia Kuwa Na Mtazamo Bora Katika Uhusiano Wetu. Ukianza Kupata Ukaribu Wa Kweli Baina Yako Na Mwenzako, Utapoteza Hisia Ya Kuhitaji Ukaribu Huo Na Mwingine Yeyote, Na Badala Yake Utaanza Kuulinda Ukaribu Mlionao.

Lengo Liwe Kuvitafuta Vile Vyote Mpenzi Wako Alivyonavyo Ambavyo Ni Kukuza Ukaribu Wenu. Mwenzako Awe Ndiyo Mtu Wa Muhimu Kuliko Wote Katika Maisha Yako.


MWANAMKE ANAHITAJI NINI........



Mwanamke Ana Upendo 98.8999% Kwa Mwanaume…Mwanamke Mpaka Kufikia Hali Ya Kukubaliana Na Wewe Na Akakuheshimu Kwa Kukuvulia Kilakitu Alichonacho Yeye Kwa Kukupa Kile Wewe Unachohitaji Kutoka Kwake Na Amekupa Heshima Wewe Kama Mpenzi Wake Umtumie Unavyokata Na Kutokana Na Mapenzi Anayokupa Anaamua Kukuamini Na Kukupa Siri Zake Zote Wewe Kama Wake Mpenzi Na Mpaka Anawatambulisha Rafiki Zake Kuwa Wewe Ni Shemeji Yao Na Hawezi Ambiwa Chochote Juu Yako Kibaya Akaacha Kukwambia, Then Leo Hii Unamdharau “Aahgghr! Hana Lolote Huyo Kwanza Malaya Tu” …(Mbaya Sana Hii, Jifunze Kuishi Kiutu Uzima Hata Kama Ana tofauti Usiwe Na Hofu Kumweleza Na Ninaimani Atakuelewa)

Usimtese Kijinsia , Usije Thubutu Kumuacha Na Kasoro Zake , Ninamaanisha Kwamba Kama Anatatizo Au Wakati Wa Mambo Yetu Yale Kuna Kitu Unataka Ufanyiwe Na Yeye, Labda Yawezekana Hajui Au Anajua Lakini Ana Walakini Kukifanya, Basi Ni Lazima Umweleze, Muweke Wazi Kumbuka Huyo Ni Mpenzi Wako Ukiwa Kimya Ukasubiri Raha Ukapewe Na Kimada Wa Nje Basi Utajikuta Siku Ya Mwisho Unaleta Ugonjwa Ndani Au Wewe Kukusababishia Kukosa Nguvu Za Kiume Unapokutana Naye Mara Nyingi Kwa Sababu Ni Chanzo Kingine Cha Kusababisha Kukosa Nguvu Unapotembea Na Wanawake Wasiohesabika, Ukikutana Naye Mara Inalala Hii Ni Kutokana Na Uchapaji Wa Too Much Nje, Kwa Sababu Unapokuwa Naye Huwezi Ku Feel Kuwa Naye. Na Badala Yake Utaanza Kuwawaza Wengine Wa Nje Ambao Hawatakusaidia Katika Kujenga Uhusiano Mwema Na Mpenzi Wako. (Kumbuka: Hata Ukibadilisha Kuni, Moto Ni Ule Ule)
Mwanamke Akikupenda Usimdharau Kama Yeye Ni Malaya… Na Mwanamke Mpaka Ukiona Hajatulia Basi Jua Tatizo Lako Wewe, Fanya Juu Chini Ili Kuweza Kumbadilisha Kwa Sababu Kumbadilisha Mwanamke Ni Kitu Kidogo Sana Kwa Sababu Umekaa Naye Muda Mrefu Na Ni Lazima Utajua Tu Umguse Wapi Aweze Kuwa Kama Mwanzo, Kama Umeshanifuatilia Kwa Mada Zangu Ninazokupa Kupitia Hapa . Na Usijeomba Mwanamke Akulilie Machozi Mbele Zako, Ameshindwa Kumlilia Baba/Mama Yake Aliyemzaa Na Amekuja Kukulia Wewe… Wewe Una Nini? Epukana Na Hili Na Utunze Heshima Yake Na Umpe Penzi Lako, Hakuna Mwanamke Mbaya/Malaya/Kicheche Ila Wewe Ndio Utafanya Awe Hivyo… Wengi Wao Wameshawahi Kufanya Haya Na Sasa Wanalia Na Kusaga Meno Kwa Sababu Walijisahau Na Mwishowe Sasa Hawajielewi Kutokana Na Maisha Wayoishi Ya Kutokua Na Chaguzi Zilizo Za Halali…

Mwanamke Anapenda Kupendwa! Mara Nyingi Wanawake Ndiyo Hasa Huwa Na Mapenzi Ya Dhati Zaidi Kuliko Wanaume. Mwanamke Anapoamua Kuwa Na Mpenzi Wake, Humpenda Kwa Moyo Wake Wote, Hivyo Hupenda Kuwa Salama Katika Penzi La Dhati Kwako.

Anapenda Uhuru, Anapenda Kujisikia Wazi Kwako Mahali Popote. Mwanamke Anajisikia Vibaya Sana Anapokuwa Hana Uhuru Hata Wa Kukushika Mkono Mnakuwa Barabarani Pamoja. Anapenda Penzi La Uwazi!

Maana Mwingine Utakuta Akikutana Na Rafiki Yake, Badala Ya Kumtambulisha Vizuri Kama Mpenzi Wake, Anaanza Kupatwa Na Kigugumizi. Utamsikia Akisema: “Ah! Huyu Ni Rafiki Yangu Bwana, Anaitwa Latipha....”Hili Ni Kosa Kubwa Linalofanywa Na Wanaume Wengi Bila Kujua Ni Kosa.

Mwanamke Anakosa Amani Ya Moyo Kutokana Na Unavyomtafsirisha Mbele Ya Rafiki Zako. Anahisi Hayupo Salama. Lazima Atajiuliza Maswali, Kwanini Hataki Kunitambulisha? Kwanini Anashindwa Kusema Mimi Ni Mpenzi Wake? Sifananii? Sina Mvuto Au Nina Tatizo Gani?

Hayo Yanaweza Kuwa Maswali Yatakayomuumiza Sana Kichwa Mpenzi Wako, Ambaye Si Ajabu Akafanya Maamuzi Ambayo Hutayapenda. Kidonda Hiki Hubaki Moyoni Mwa Mwanamke, Huwa Vigumu Sana Kuonyesha Wazi Kwamba Amechukia Kutokana Na Uliyomfanyia, Lakini Atabaki Akiugulia Moyoni Mwake Kwa Uchungu.
Hata Hivyo, Kinachokuja Akilini Mwake Ni Kutafuta Mwanaume Mwingine Ambaye Atakuwa Wazi Kwake Ili Aweze Kufurahia Mapenzi Badala Ya Kuendelea Kuumia Moyoni Mwake. Ni Dhahiri Kwamba Uamuzi Huu Hautaufurahia Hakika.
1. UNAVYOJALI...
Mwanamke Anapenda Awe Wa Pekee Kwako, Umsikilize, Umjali Na Umpe Kipaumbele Katika Kila Unachokifanya . Wanawake Wengi Wanapenda Kudekezwa, Lakini Hawapendi Kuweka Hilo Wazi Kwa Mwanaume Wake. Kwa Kumtazama Tu Utagundua Mpenzi Wako Anahitaji Nini Zaidi Kwako!

Wakati Mwingine Anaweza Kukupa Mitihani Ili Kupima Kiwango Cha Penzi Lako. Anaweza Kukuambia Anaumwa Au Anauguliwa Na Mtu Wake Wa Karibu, Lengo Ni Kuangalia Ni Jinsi Gani Unakuwa Makini Anapokuwa Na Matatizo.

Vile Utakavyochukulia Tatizo Lake Kwa Ukaribu, Uchungu Na Kuona Kama Lako, Ndivyo Utakavyomfanya Aone Thamani La Penzi Lako Kwake, Ikiwa Vinginevyo Basi Humuacha Na Machungu Moyoni, Huku Akijutia Kuwa Na Mpenzi Wa Aina Yako.

Hii Ni Siri Ambayo Si Rahisi Mwanamke Wako Akueleze Moja Kwa Moja. Atatumia Lugha Ya Ishara Kuonesha Jinsi Ambavyo Anahitaji Kuwa Wa Pekee Kwako.

2. JIFUNZE SIRI HIZO.....

Hapa Ndipo Mwanaume Mwerevu Anatakiwa Kuwa Makini, Ni Lazima Ufahamu Siri Zilizopo Moyoni Mwa Mpenzi Wako. Jifunze Kusoma Hisia Za Mpenzi Wako Kwa Nje, Kabla Ya Kufanya Kitu, Fikiria Mara Mbili, Lakini Baada Ya Kufanya, Msome Kupitia Uso Wake.

Analifurahia Au Umemchukiza? Ni Vizuri Kugundua Hilo Ili Uweze Kufunga Hisia Za Kumfanya Aanze Kufikiria Kukusaliti. Hata Mnapokuwa Faragha Ni Vizuri Kuwa Makini Na Kila Unachokifanya! Chunguza Kama Anafurahia Penzi Lako Na Manjonjo Yote Unayomfanyia.

Kumbuka Kwamba Ni Vigumu Sana Mwanamke Kukueleza Moja Kwa Moja Kwamba Hujamfurahisha Au Kuna Kitu Umekikosea, Hii Husababishwa Na Hofu Ya Kuogopa Kukufanya Ujisikie Vibaya.

Kwa Maneno Mengi WEWE Mwanaume Ndiye Mwenye Kazi Ya Kuangalia Mwanamke Wako Anapenda Nini Na Nini Hapendi Ili Uweze Kuwa MWANAUME Wake Bora, Maana Hata Hisia Zake Za Ndani Utakuwa Unazifahamu. Ni Rahisi Sana, Soma Kupitia Macho Yake Kila Unachomfanyia, Utaujua Ukweli. Unajua Hata Ukimwita Kwa Jina Ambalo Hana Msisimko Nalo Lakini Ukiwa Unamtazama Usoni Ni Rahisi Sana Kugundua Kitu Fulani, Kama Hajakipenda Utaona Kwenye Macho Na Akikipenda Pia Utaona.

Unapokuwa Naye Faragha, Tumia Uwezo Wako Wote, Lakini Kumbuka Kwamba Si Kila Utakachokifanya Utamfurahisha. Hii Inamaanisha Kwamba, Baada Ya Kumchunguza Jinsi Anavyosisimka, Utaweza Kugundua Wapi Kuna Msisimko Zaidi Kuliko Sehemu Nyingine.

Hapo Sasa Unaweza Kuibuka MSHINDI Maana Utakuwa Umeziweka Siri Zake Hadharani, Kwa Maneno Mengine Kama Yeye Aliona Siri, Basi Umeweza Kuzigundua Na Angalau Umeanza Kuzifanyia Kazi. Nawapenda Sana Rafiki Zangu, Ndio Maana Nawapeni Mambo Mazuri Na Yenye Sifa Ili Msiweze Kusababisha Kitu Kinaitwa..."UMENITENDA/AMENITENDA" (KUTENDANA NI DHAMBI KUBWA SANA) NIWATAKIE SIKU NJEMA..

WAZO LA LANGU LEO:

WANAWAKE: Napenda Kuwashauri Wanawake Wote Ambao Wapo Katika Mahusiano Ya Kimapenzi Wajaribu Kuwa Wabunifu Katika Mapenzi, Mpe Mpenzi Wako Mapenzi Yote Toka Moyoni Mwako. Usidanganywe Kuwa Mapenzi Ni Mitishamba Hakuna Dawa Ya Mapenzi Kwa Mganga Ila Dawa Unayo Wewe Mwenyewe Mridhishe Mpenzi Wako Kwa Kumpa Vitu Vipya Katika Mapenzi Halafu Uone Je, Penzi Lako Kwa Mwenza Wako Utachangia Na Wenzako?!

WANAUME: Siku Zote Uwapo Katika Mapenzi Fahamu Kuwa Unapaswa Kumridhisha Mpenzi Wako Katika Tendo Mfanye Ajisikie Raha Pindi Muwapo Chumbani Inakubidi Uwe Mwanamke Wa Kileo Ujitahidi Kuwa Mbunifu Katika Mapenzi Kwa Kujituma Pindi Mnapokuwa Chumbani Na Mpenzi Wako, Jaribu Kushughulika Tumia Viungo Vyako Vya Mwili Katika Kuamsha Hisia Za Mwandani Wako Kabla Ya Kuanza Nae Kufanya Mapenzi Ili Kuhakikisha Mpenzi Wako Anapata Raha Na Inakuwa Ni Njia Nzuri Ya Wewe Kumfanya Mpenzi Wako Ahisi Kuwa Wewe Ni Muhimu Kwake.