Saturday 26 October 2013

TACAIDS; WANAOSAMEHE HAWAPATI MAAMBUKIZI YA VVU




Afisa utafiti wa tume ya kudhibiti Ukimwi nchini(TACAIDS) Dr. Avoldia Mlokozi. 



Na Gordon Kalulunga, Mbeya



TUME ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS) imesema wanandoa na watu walio kwenye mahusiano, wakiwa na tabia ya kusameheana wanapokoseana, wanaweza kupunguza ongezeko la maambukizi ya VVU.



Hayo yalisemwa na afisa utafiti wa tume hiyo Dr. Avoldia Mlokozi alipozungumza na waandishi wa habari Jijini Mbeya katika mohojiano maalum.



‘’Ukitaka kuishi kwa usalama ni kuwa na msamaha kwa mwenzako badala ya kuchepuka kwenye ndoa kwa kisingizio cha kuudhiwa na mwenza wako’’ alisema Dr. Mlokozi.



Alisema katika kanda ya nyanda za juu kusnini magharibi, kiwango cha maambukizi ya VVU, mkoa wa Mbeya una asilimia 9, Rukwa 6.2 na Katavi ni 5.9 kiwanga ambacho ni kikubwa kuliko wastani wa taifa wa asilimia 5.1.



Alitanabaisha kuwa katika maambukizi hayo, wanawake ndiyo walioathirika zaidi kwa kuwa na maambukizi ya wastani wa asilimia 9.2 na wanaume asilimika 6.5 kwa takwimu za utafiti wa mwaka 2011-2012.



‘’Wanawake wanaopata zaidi ugonjwa huo ni wale wenye umri wa miaka kati ya 20 mpaka 30 kwasababu hao ndiyo wanakuwa kwenye mahusiano, kuolewa na kujifungua’’ alisema Dr. Mlokozi.



Aliongeza kwa kusema kwamba, tayari kuna mikakati ya elimu kwa lika hiyo ili kuweza kupunguza ushamiri wa maambukizi hayo ya VVU kwa wanawake.



Kuhusu mkoa wa Mbeya, alisema mkoa huo umeendelea kuathirika zaidi  na ugonjwa huo kutokana na mwingiliano wa watu kimaendeleo ikiwemo suala zima la uchumi ambapo baadhi ya wafanyabiashara na madereva wanaotumia barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam na kwenda Zimbabwe, Malawi, Zambia, Kongo na kwingineko kusini mwa Afrika, wanalala katika mkoa huo na kujiingiza katika mahusiano na baadhi hawatumii Kondomu.



‘’Nchi hizo zina maambukizi kuliko ya hapa nchini, hivyo pia ni moja ya sababu ya kuendelea kushamiri ugonjwa huo mkoani Mbeya na baadhi ya wanaume hawajafanyiwa tohara ambayo inasaidia kupunguza maambukizi kwa asilimia 60 na magonjwa ya zinaa’’ alisema Dr. Mlokozi.

No comments:

Post a Comment