Thursday 20 February 2014

WABUNGE WA KATIBA MPYA KUTAKA NYONGEZA ZA POSHO, SIRI NZITO YAFICHUKA


*Wabunge wa Jamhuri wadaiwa kuwa kichocheo
Kalulunga blog team, Dodoma.

SIKU moja baada ya wabunge maalum wa bunge la katiba kulalama na kutaka kuongezewa posho, uchunguzi umebaini kuwa shinikizo hilo linatokana na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



Baadhi ya Wabunge hao wa Jamhuri, wanadaiwa kusukuma jambo hilo kwa maslahi yao binafsi na kwa malengo yao ambayo tayari yamebainika.



Malengo yaliyotajwa na vyazo vyetu vya habari, vimesema kuwa wabunge hao wanashinikiza wabunge wa bunge maalum waongezewe posho kutoka kiwango cha sasa cha Tsh. 300,000 mpaka kufikia kiasi cha Tsh. 540,000 kwa siku.



Vyanzo hivyo vinahoji iweje wabunge hao walioomba kufanya kazi hiyo kwa maslahi ya taifa wadai kiasi hicho kikukwa cha fedha!



‘’Hawa wamekuja hapa kwa maslahi yao na hata katiba itakayopitishwa hapa itakuwa kwa maslahi yao na wala si wananchi’’ kilihoji moja ya chanzo chetu kutoka miongoni mwa walengwa wanaopinga ongezeko la posho hizo.



Aidha uchunguzi umebaini kuwa, nia kuu ya wabunge wa Jamhuri wanaoshinikiza ongezeko la posho hiyo, wanalenga kupata mkupuo wa fedha ambazo zitawawezesha kulipa ama kupunguza madeni ya magari yao ya kifahari waliyoyakopa.



Wakati hali hiyo ipo hivyo, taarifa kutoka serikalini, zimeeleza kuwa mpaka kufikia leo, Halmashauri kote nchini, bado hazijafikishiwa fedha za maendeleo ya wananchi.



''Wanatumia mwanya wa bunge la katiba kutaka nyongeza ya posho ili kulipa madeni ya magari yao''.

No comments:

Post a Comment