Hakunaga na Brother Kalu
WAPENZI wasomaji wa safu hii niwashukuru
sana hasa wadau
wa Sumbawanga wakiwemo wanafunzi wa
ST. Maurus Chemichemi ambao mliamua kuniita kwa
ajili ya kufahamiana, hakika mlionesha moyo mkubwa wa upendo na haja ya kutaka
kujua mambo mengi kuhusu mahusiano ingawa muda haukutosha lakini ibaki historia
kuwa tulionana.
Jana tuliona dalili za mwanamke ama mazingira yanayomfanya kupenda na
kujisikia kufanya mapenzi, wiki hii kama
nilivyowajuza tuone wanaume wanapenda kuoa wanawake wenye tabia zipi.
Mtu
anaweza kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na wakati mwingine kwasababu ya
kukidhi tamaa ya ngono kisha akabaini kuwa anaona mvuto mkubwa kwa mpenzi huyo.
Upande mmoja ama pande zote zaweza kudhani kuwa mvuto huo ndiyo dalili za kuwa
na mapenzi ya kudumu jambo ambalo ni kosa na athari zake huonekana baadae.
Sasa
tukijite kwenye kitovu cha mada tajwa hapo juu ambapo wanaume wengi wanaojua
athari za kukurupuka kuoa wanapofikia hamu ya kuoa si kwamba wanakurupuka bali
huwachukua muda mrefu kuchunguza hata kama
wataona wanawake wazuri wa sura.
Hapa
ni kipindi kigumu sana kwa wanaume na wanawake wengi hujidanganya na kufikiri
kuwa kitu kinachoweza kuwashawishi wanaume kuwa nao kwa ndoa ni kujiremba
kupindukia hivyo wengi huishia kupoteza muda na gharama kubwa na kusahau kuwa
kuolewa ni zaidi ya uzuri wa sura na kujiremba.
Hapo
awali mwanamke mwenye umbo zuri na sura nzuri alikuwa na asilimia zaidi ya 90
za kuolewa lakini hali imebadilika ambapo wanawake wenye sura nzuri na maumbo
mazuri wamekuwa ni wanawake wa kustarehesha wanaume na kupungukiwa sifa za
kuolewa ambapo wanaume wengi wanasema kuwa wakiwaoa ni wasumbufu na wana viburi
kutokana na kutongozwa na wanaume wengi hivyo kujiona kuwa soko lake ni kubwa
hata akiachika.
1.Mapenzi Mema yenye faraja si makwazo
Lengo
kubwa la mwanaune kuoa ni kupata mapenzi ya kweli na faraja kutoka kwa mkewe na
hatimaye kupata watoto ambao wataongeza faraja katika familia na hatimaye
kujivunia katika jamii mnayoishi.
Kumekuwa
na tabia za wanawake wengi kupenda sana
matukio kwamfano wengi wao wanapenda kuonekana wameolewa lakini maisha ya ndoa
hawayataki na hawa tunawaita wanawake wazugaji na baadhi wanapenda pesa za
mwanaume ama kuonekana yupo na Fulani.
Wengi
wao hawajui kuwa maisha yanabadilika waweza kuwa nacho leo na kesho ukakosa na
kusahau kuwa maisha ya ndoa kila uchwapo yanatakiwa kutawaliwa na upendo.
Niwakumbushe
wanawake mambo walau matatu yanayoweza kuboresha mahusiano na maisha ya ndoa
ambayo ni neno Samahani, pole na Asante yakizingatia hayo
yatakusaidieni.
2. Mwanamke mwenye tabia Njema
Mwanamke
ukiwa na tabia njema kwa kujitambua kuwa wewe ni mwanamke tayrai unakuwa
umejiweka katika asilimia kubwa ya kuolewa na mwanaume wa ukweli mwenye uhitaji
wa kuwa na mke maana tabia njema waswahili wanasema ni silaha.
Hakuna
asiyejua umuhimu wa silaha na ndiyo maana wenzetu wazungu walio wengi
wanathamini sana
wapisgi na walinzi wao maana hao wameshika asilimia Fulani za uhai wao.
Linapokuja
suala la kuoa hakuna mtu anayeuliza kuwa mwanamke anayetaka kuolewa ana kimo
gani ama umbile likoje bali kitu cha kwanza kuuliza ni tabia watu wanaulizana
ama kuambia kuwa je unaijua tabia yake? Na je unaona mtawezana na huyo mbona
chakaramu huyo? Huku wengine wakisema aaaaaa.. pale umepata mke ana tabia nzuri
sana na
anaheshimu mkubwa na mdogo na anamisimamo.
Wapo
wanaume walikurupuka kuona wanawake wenye sura na maumbile mazuri lakini baada
ya siku chache kilichotokea ni machafuko makubwa na hatimaye ndoa zikavunjika
na hawatamani tena hata kuwa na mahusiano ya kawaida na wanawake warembo.
3. Wenye kupenda kutoa ushauri wa
kimaendeleo.
Kuna
tabia mbili ambazo wanaume wanapenda kuziona kwa wanawake ambao wanatamani
kuwaoa. Wanaume wengi kwa sasa hawapendi kuoa mwanamke ambaye hana kazi na
vinginevyo mwanamke huyo atakuwa na mawazo chanya ya kimaendeleo.
Mwanamke
mwenye fikra za kumshauri mwanaume wake masuala ya kimaendeleo na mwenye
kujituma bila manug’uniko na kutoa lawama hata kwa vitu vidogo alivyotendewa na
mpenzi wake ana nafasi kubwa ya kuolewa kuliko ambaye ana ajira yake kwasababu
mawazo ni dira ya kila jambo.
Hapa
sizungumzii mwanamke ambaye anapenda kunyoosha miguu nyumbani na kuagiza ama
kupanga mambo ambayo anataka afanyiwe na mtu mwingine, la hasha bali
nazungumzia mwanamke ambaye anapenda kumshirikisha mwenzi wake jambo ambalo
wanaweza kulifanya kwa pamoja ama kupanga kwa ajili ya maendeleo yao na jamii
inayowazunguka ikiwemo kutoa misaada kwa wahitaji ama kutembelea wagonjwa
Hospitalini.
Mwanaume
hapendi kuwa na mwanamke ambaye anapenda makuu, si unajua kuna wanawake si
vijijini wala mijini wao makuu kwao ndo maisha, na hapa nitoe dawa inayoitwa limbwata,
limbwata linalotakiwa hapa ni kwamba wanaume kama watoto wanapenda sana
kunyenyekewa na hilo ni limbwata baaab kubwa hivyo mwanamke haupaswi kupenda
makuu ni moja ya dalili inayokukosesha kuolewa ama kuaminika katika jamii
unayoishi na kama upo kwenye ndoa tambua mwanaume wako anaporudi nyumbani
anaona kama anaenda Rumande.
4. Wanawake wavumilivu
Wapo
wanawake ambao si wavumilivu hata chembe katika maisha, wao akili zao zimeganda
kuwa maisha yanasonga mbele bila kujua kuwa kuna wakati wa majaribu lakini kila
jaribu lina mlango wa kutokea maana katika maisha ama katika mahusiano kuna
matatizo ya kiafya na hata kukwama kabisa kifedha kwa mwanaume ambapo wengi
wetu husfikia hatua ya kusinyaa ni kutokana na mawazo.
Matatizo
ya kiafya au ukosefu wa fedha ni moja ya wakati wa kipimo kwa kutambua mwanamke
mvumilivu ama matatizo mengine si tumeshuhudia wengi wakiwatoroka waume zao na
kuachanana wapenzi wao kisa matatizo jambo ambalo kwa mwanamke wa namna hiyo
hujidhihilisha kuwa hana sifa ya kuwa mke wa Mtu.
Baada
ya kuona baadhi ya tabia ambazo wanaume wengi wanapenda wazione kwa wanawake
wanaotaka kuwaoa, wiki ijayo tutaona ni vitu gani muhimu vinavyotakiwa kuwepo
kabla ya kufanya mapenzi.
Teta nami kupitia
0655 440749
No comments:
Post a Comment